logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kate Actress amesherehekea bintiye

Kate alimwandikia bintiye ujumbe akimtakia heri ya kuzaliwa

image
na Radio Jambo

Makala15 December 2022 - 07:28

Muhtasari


β€’ "Ni siku ya Njeri! Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu. Kile ambacho husemwa kuhusu tufaha na mti. Ni binti wa mama yake, tabia kama zake! Heri ya kuzaliwa binti yangu, roho yangu, rafiki yangu," Kate aliandika.

Muigizaji Kate Actress amemsherehekea bintiye, Njeri leo anapofikisha miaka mitatu tangu kuzaliwa.

Kwenye Instagram, Kate alimwandikia bintiye ujumbe wa kumtaki heri ya kuzaliwa na kupakia picha zake.

"Ni siku ya Njeri! Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu. Kile ambacho husemwa kuhusu tufaha na mti. Ni binti wa mama yake, tabia kama zake! Heri ya kuzaliwa binti yangu, roho yangu, rafiki yangu," Kate aliandika.

Mama huyo alizidi kujivunia binti yake kwa kupakia picha mbalimbali ambazo alipigwa kwa ajili ya siku hii.

"Umejuaje Kate ni mama yangu? Umenichizisha Njeri. Asante kwa kunichagua. Bosi wangu mdogo wa kike," muigizaji huyo alisema.

Mumewe Kate pia hakusita kumsherehekea binti yao kwa ujumbe na kumshukuru mkewe kwa kumlea.

"Malkia wangu amefikisha miaka 3πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸ₯³πŸ₯³πŸ₯³. Miaka 3 nimejifunza kujitolea kutoka kwako. Zaidi ya miaka 100 NjeriπŸ₯‚. Kate Actress, asante kwa kumlea binti yetu," Phil Director alisema.

Muigizaji huyo amebarikiwa na watoto wawili, wa kike na wa kiume, ambapo wa kiume alifikisha miaka 16 mwezi wa Julai.

Kate alichukua fursa hio kumsherehekea mwanawe kwa ujumbe mrefu hukua akimtakia heri ya kuzaliwa.

"Kheri za siku ya kuzaliwa mwanangu, nina mengi ya kusema lakini najua ulisema hakuna jumbe ndefu na picha za aibu. Nitaheshimu hilo, wewe mtu mzima mwenye ndevu mbili .Wewe ni motisha wangu toka siku ya kwanza , natumai nimetimiza ahadi zangu kwako , nakupenda sana na ninajivunia wewe hadi sasa πŸ€—πŸ™πŸ½ . Sasa naomba uende maji nyasi ukimaliza osha mabati,," Kate aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved