Stephen Letoo adhibitisha kuwa miongoni mwa waliokula sumu, asema yuko sawa

Wafanyikazi wa Royal Media waliripotiwa kula chakula kilichodhaniwa kuwa na sumu siku ya Krismasi.

Muhtasari

• Kampuni binafsi ya kupakua vyakula iliwapatia wafqanyikazi wa kampuni ya Royal Media  chakula siku ya Krismasi.

• Baadae wafanyikazi hao walianza kulalamika maumivu ya tumbo katika kile kilidhaniwa kuwa sumu kwenye chakula hicho.

Ripota Stephen Letoo
Ripota Stephen Letoo
Image: Facebook

Ripota wa runinga ya Citizen Stephen Letoo amedhibitisha kuwa sasa amepata nafuu na yuko salama na imara baada ya wafanyikazi wa kampuni ya Royal Media ambayo ni mzazi wa kituo cha Citizen kudai kula chakula chenye sumu siku ya Krismasi.

Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Wachira Waruru alitoa taarifa wazi ya kukiri kutoa kwa tatizo hilo ambalo liliwakumba wafanyikazi wote ambao walikuwa wanafanya kazi zamu ya Krismasi kutoka ofisi zao zilizopo Nairobi.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kampuni hiyo iliitisha chakula kutoka kwa kampuni moja ya kusambaza vyakula kwa ajili ya wafqanyikazi waliokuwa kazini siku ya Krismasi lakini ilipofika siku ya Boxing ambayo ni siku moja baada ya Krismasi, wafanyikazi hao wote walianza kulalama maumivu ya tumbo na kukimbizwa katika hospitali mbali mbali Nairobi.

Kwa bahati mbaya taarifa hiyo iliai kuwa mmoja wa wafanyikazi hao ambaye ni mwanamke alifariki kutokana na tukio hilo lililokisiwa kuwa ni jaribio la sumu kwenye chakula.

Mashabiki mbali mbali walifurika mitandaoni kuwatakia wafanyikazi wote nafuu ya haraka huku kukiwa hakujulikani ni akina nani waliathirika na tukio hilo la bahati mbaya.

Letoo Jumatano jioni baada ya siku kama mbili za kimya aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kudhibitisha kuwa sasa yuko sawa – ujumbe ulioeleweka na wengi kuwa huenda alikuwa mmoja wa waathirika lakini kwa huduma za kimatibabu alipata nafuu.

“Sasa niko sawa,” Letoo alisema.

Watu mbalimbali walimtakia kuendelea kupata nafuu kwa haraka huku wengine wakikashfu tukio hio ambalo bado linazidi kuchunguzwa ili kupata ukweli kuhusu sumu inayodaiwa kuwekwa kwenye chakula hicho.

“Baada ya kuzungumza na wewe jana, ilibidi niseme ombi kwa ajili yako. Vizuri kusikia kuwa sasa uko salama,” Philip Etale alimwambia.

“Amina!! Nimefurahi kusikia haya, yeyote anayesoma hii, kuwa mwangalifu adui yako anaweza kuwa mtu ambaye yuko karibu na wewe kila wakati!” mwingine alisema.

“Tunamshukuru Mungu kwa afya yako na wengine wengi ambao bado hawajapona, Mungu awatembelee kwa jina la Yesu” Nyambeki aliandika.