logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gari la Crazy Kennar lakwama kwenye matope kijijini mwao Awasi, kaunti ya Kisumu (Video)

Alilazimika kuita huduma za trekta kulivuta gari hilo kutoka kwa matope.

image
na Radio Jambo

Makala31 December 2022 - 12:09

Muhtasari


β€’ Mchekeshaji huyo alisema alikwama kweney matope kwa saa kadhaa mpaka giza likaingia na kuita trekta kusaidia kulitoa gari kwenye matope.

Mchekeshaji wa mitandaoni Crazy Kennar kama Wakenya wengine msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya alitembea kwao kijijini kwa kutumia gari lake la kifahari Landcruiser Prado TX.

Kufuatia mvua nyingi ambazo zinaendelea kunyesha kote nchini, na ubovu wa barabara nyingi za vijijini, gari la msanii huyo lilikwama kwenye barabara moja ya matope ambayo ilikuwa imechafuka kwa maji yaliyokwama pamoja na matope mengi.

Katika video ambayo Kennar alipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, vijana kadhaa wa kijijini mwao wanaonekana wakijaribu kumsaidia kulisukuma ari lake kulikwamua kutoka kwa matope lakini juhudi zao zote ziliambulia patupu.

Kennar alisimulia jinsi alipata matatizo kulikwamua gari hilo kutoka kwa barabara ya matope huko Awendo mpaka giza likaingia kama bado amekwama njiani na si kwa sababu ya msongamano wa magari kama ambavyo amezoea Nairobi bali safari hii matope na barabara mbovu ndivyo vilimkwamisha.

“Kwa hivyo nilikwama kwa saa 4 nikienda nyumbani Osiri Kanyipola - Ahero Magendo Katambo makutano Community Cess Rd. Kujiunga na Jumuiya za Kanyipola, Kochogo na Kakola. Mbunge wa eneo na MCA fanyeni kitu, mahari ya warembo itakwama jameniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kweli CC iliteseka. Mapambano,” Kenner alifuatisha maelezo hayo kwenye video ile.

Mwishowe kiza kilipobisha, Kenner alilazimika kutafuta huduma za trekta ambalo lilifika hapo na kuvuruta gari hilo kuliondoa kwenye rundo la matope.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved