logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Esther Musila asherehekea mwaka mmoja wa ndoa na Guradina Angel, "Kila siku ni fungate!"

"Asante kwa kunionyesha unyenyekevu na kuwa baraka kwa maisha yangu" - Musila.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 January 2023 - 09:27

Muhtasari


  • • Ndoa ya wawili hao iligonga vichwa vya habari haswa kutokana na utofauti uliopo baina ya umri wa Guardian Angel mwenye miaka 31 na Musila mwenye miaka 53.
  • • "Safari hii imekuwa nzuri, mimi bado ni mchumba wako, wewe bado ni bwana harusi wangu." - Musila
Musila na Angel washerehekea mwaka mmoja wa ndoa

Esther Musila, ambaye ni mke halali kabisa wa ndoa kwa mwanamuziki wa injili Guardian Angel amejawa na furaha akisherehekea mwaka mmoja tangu kufunga ndoa na mumewe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Musila ameibua kumbukumbu kuwa mwaka jana Januari tarehe 4, tarehe sawa na leo, alisema ‘ndoa’ kwa ombi la Guardian Angel na kula yamini mbele ya umati mchache wa watu ambao walijitokeza kushuhudia tukio hilo ambalo ni la kupendeza machoni pa Mungu.

Musila alipakia picha za kipindi hicho akisema kuwa uamuzi wa maana kabisa alioufanya mwanzoni mwa mwaka 2022 ni kukubali kuolewa na rafiki yake wa karibu mno – Guardian Angel.

Alisema kuwa katika hadithi za kimapenzi zote duniani ambazo zitasimuliwa, basi yao itakuwa hadithi ya kuyeyusha moyo wake muda wote na siku zote.

“04.01.2022...Mwaka mmoja uliopita katika siku hii, nilifunga ndoa na rafiki yangu mkubwa na kati ya hadithi zote za mapenzi duniani, hadithi yetu itakuwa ni kipenzi changu daima. Safari hii imekuwa nzuri, mimi bado ni mchumba wako, wewe bado ni bwana harusi wangu. Mwaka mmoja umepita lakini bado ni kama fungate...” Musila aliandika.

Musila alimsifia mumewe Guardian Angel na kumtaja kuwa mwanaume anayejua thamani ya mapenzi na ambaye amefanya uhusiano wao kuwa rahisi kabisa kuendelea huku akimuahidi mapenzi yasiyojua ukomo.

“Kila siku nakupenda zaidi ya siku iliyopita. Unafanya Mr & Mrs kuonekane rahisi sana.... Heri ya kumbukumbu ya miaka mpendwa wa maisha yangu na mengine mengi yajayo.🥂🥂🥂 Nakupenda Bwana Omwaka,” Musila alisema.

Musila pia aliendelea mbele na kumuandikia Guardian Angel ujumbe mtamu akimshukuru kwa vicheko visivyo na mwisho mpaka usiku wa manane.

“Mpenzi wangu, moyo wangu umejaa shukrani kwa upendo na urafiki unaotoka kwako. Asante kwa vicheko vya usiku wa manane na busu za asubuhi unazoniogesha nazo. Asante kwa kunionyesha unyenyekevu na kuwa baraka kwa maisha yangu. Kila dakika ya maisha yangu na wewe imekuwa ya kukumbukwa,” alisema.

Ndoa ya wawili hao iligonga vichwa vya habari haswa kutokana na utofauti uliopo baina ya umri wa Guardian Angel mwenye miaka 31 na Musila mwenye miaka 53.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved