Furahia maisha, kuna wakati mwingi wa kufa - Mpenzi wa Mungai Eve, Trevor ashauri

Baadhi walimwambia ametoa ushauri huo wakati wa Januari ambapo tafrija ni haba.

Muhtasari

• “Furahia! Kuna wakati mwingi wa kufa,” Director Trevor aliandika kwenye Instagram yake.

Trevor na mpenzi wake Mungai Eve
Trevor na mpenzi wake Mungai Eve
Image: Instagram

Director Trevor ambaye ni mpenzi wa mwanablogu wa YouTube Mungai Eve ametoa sababu zake kuhusu ni kwa nini watu wanastahili kujivunjari na kuburudika kwa maisha.

 Trevor alitoa ushauri wa ajabu ambapo aliwaambia watu kuwa katika maisha ukiwa hai hufai kukosa sababu ya kujivinjari kwani mbeleni kuna muda mwingi tu wa kuwa maiti asiyeweza kujisogeza wala kujihudumia.

“Furahia! Kuna wakati mwingi wa kufa,” Director Trevor aliandika kwenye Instagram yake.

Licha ya ushauri wake kuonekana wa maana kwa kiasi fulani, wengi walionekana kumsuta kuwa aliutoa wakati ambao ni mbaya – Januari.

Huu ni wakati ambao kwa Wakenya wengi ni mpito wa majaribu mengi ya kupambana na ghadhabu ya ugumu wa maisha, haswa kwa wale ambao walitumia hadi senti ya mwisho katika tafrija za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Ushauri mzuri sana huu lakini sema nini dingi... umeusema wakati mbaya sana...Januari hakuna kakiru,” mmoja alisema.

“Maisha yetu si huweka kwa mikono ya Mungu,” Mwingine kwa jina Denno alisema.

Kijana huyo ambaye anashirikiana na Mungai Eve katika kuzalisha video za udaku kwenye mtandao wa YouTube amekuwa akijipata katika zogo la mitandaoni pamoja na mpenzi wake. Watu wamekuwa wakiwashauri kuendeleza furaha hiyo yao katika kupata mtoto kutokana na dhana hiyo hiyo kuwa maisha ni mafupi.

“Haya basi tumeelewa muda wa kufa ni mwingi, nanyi fanya hima muongezeka kwa familia,” mwingine alimwambia akilenga pale pale katika suala la wao kupata mtoto.

Mungai Eve aliwahi kuwakaripia wale waliokuwa wanawawekea shinikizo la kupata mtoto huku akiwataka kutoingilia mambo yao ya kibinafsi kwani kupata mtoto ni uamuzi wa kibinafsi kwa mtu.