Chifu aliyerekodiwa akidensi klabuni adai alikuwa akichunguza matumizi ya dawa za kulevya

Migun alisema alikuwa ameenda kuchunguza janga la utumizi wa dawa za kulevya.

Muhtasari

•Chifu Msaidizi ambaye video yake akicheza densi kwa ustadi katika kilabu ilivuma kwenye mitandao ya kijamii, amesema alikuwa ameenda kufanya kazi ya siri.

•"Nilipokuwa nikicheza, mtu niliyekuwa naye alinirekodi na sikutarajia kwamba ingeenea mtandaoni." Alisema.

, Chifu Msaidizi wa eneo moja katika Kaunti ya Kisumu amesema alikuwa kwenye kazi ya siri katika klabu.
John Ogilo Migun , Chifu Msaidizi wa eneo moja katika Kaunti ya Kisumu amesema alikuwa kwenye kazi ya siri katika klabu.
Image: HISANI

John Ogilo Migun, Chifu Msaidizi wa eneo moja katika Kaunti ya Kisumu ambaye video yake akicheza densi kwa ustadi katika kilabu ilivuma kwenye mitandao ya kijamii, amesema alikuwa ameenda kufanya kazi ya siri.

Katika mahojiano na Citizen Digital, Migun alisema alikuwa ameenda kwenye klabu hiyo kuchunguza janga la utumizi wa dawa za kulevya.

"Baada ya kazi, tulikua tumeenda mambo ya undercover kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, ghafla wimbo ambao napenda ukachezwa, nafahamu huo mziki na naupenda," alisema.

Migun alisema alipokuwa akinengua kiuno, kijana aliyekuwa naye alianza kumrekodi na hakujua kuwa video hiyo ingesambaa mitandaoni.

"Nilipokuwa nikicheza, mtu niliyekuwa naye alinirekodi na sikutarajia kwamba ingeenea mtandaoni." Alisema.

Aidha alieleza kuwa video hiyo imemsaidia kutangamana na vijana, hivyo kuwapa uhuru wa kufunguka kwake kuhusiana na masuala yanayowahusu.

“Tangu video hiyo kusambaa, nimekuwa nikitangamana na vijana kwa uhuru, wanakuja ofisini kwangu bila woga kunieleza masuala yao,” alisema.