Laventa Amutavi aonesha picha adimu ya mumewe Omanyala ndani ya gwanda la kijeshi

Amutavi alisema kushuhudia mumewe akikwea ngazi za mafanikio kunamtia furaha ya moyoni isiyoweza kuelezeka.

Muhtasari

• Omanyala alishinda dhahabu katika mbio za mita 100 kwenye mashindano ya Commonwelath Agosti mwaka jana.

•Japo ni polisi kutokana na hadi yake ya kuwa mwanariadha, Omanyala hajawahi onekana akiwa amevalia sare za kijeshi mpaka pale mkewe alipovujisha picha hiyo.

Laventa apakia picha adimu ya Omanyala ndani ya gwanda la jeshi
Laventa apakia picha adimu ya Omanyala ndani ya gwanda la jeshi
Image: Instagram

Mpenzi wa mwanariadha mwenye mbio zaidi barani Afrika, Ferdinand Omanyala, Laventa Amutavi amemsherehekea mpenzi huyo wake kwa mafaniko makubwa haswa mwaka uliopita.

Amutavi alionesha furaha yake kwa kupakia picha adimu ya mwanariadha huyo akiwa katika sare rasmi ya jeshi la polisi nchini.

Mwanadada huyo ambaye pia ni mwanariadha chipukizi alimwaga makopakopa kweney picha hiyo huku akisema kuwa amekuwa shahidi mkubwa katika safari ya mumewe Omanyala katika riadha ambapo katika miaka miwili iliyopita amepata umaarufu mpaka kukabidhiwa kazi katika jeshi.

“Kuadhimisha kile ambacho Mungu amekutendea mpenzi wangu. Mungu amekuwa mwaminifu; kushuhudia tu onyesho hili lisilo la kawaida huhisi moyo wangu kwa furaha na shukrani. Hongera na cheers kwa baraka zaidi,” Amutavi aliandika.

Mwanariadha huyo ambaye alifanikiwa kutinga nusu fainali ya mita 100 katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 iliyocheleweshwa, na baadae akashiriki mashindano ya Oregon nchini Marekani ambapo pia hakufanikiwa kuibuka miongoni wa watatu bora.

Hata hivyo, wengi walilaumu matokeo yake duni katika mbio za Oregon kufuatia masaibu yaliyokumba safari yake ambapo hati yake ya usafiri ilikuwa na migogoro kupelekea kuondoka nchini kwa kuchelewa.

Mwanariadha huyo aliipandisha hadhi yake aliposhiriki katika mashindano ya Commonwealth na kuibuka mshindi wa dhahabu.

Hata hivyo, bado inasalia kuwa ndoto yake kuu kuibuka mshindi wa mbio za mita 100 katika mashindano yenye hadhi yake kama yale ya dunia ya IAAF au mashindano ya Olimpiki, kwani yale ya Commonwealth washiriki huwa tu kutoka mataifa ambayo yalikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza pekee.