Anerlisa apewa zawadi za saa ghali na Iphone, baada ya kusema maua si zawadi

Anerlisa alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 35.

Muhtasari

• Wow, ahsante wote mliofanikisha siku yangu ya kuzaliwa kwa zawadi nzuri. Shukrani zangu za dhati kutoka moyoni - Anerlisa.

Amerlisa Muigai asema maua si zawadi katika harusi
Amerlisa Muigai asema maua si zawadi katika harusi
Image: instagram

Mrithi wa kampuni ya kutengeneza na kuzaa vileo ya Keroche, Amerlisa Muigai siku mbili zilizopita alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Marafiki wake mbali mbali waliohudhuria tafrija hiyo walimkabidhi zawadi kochokocho ambazo mrembo huyo hajasita kuzifurahia kwa kuzionesha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Anerlisa ambaye alisemekana kufikisha miaka 35 alionesha baadhi ya zawadi ambazo alipatiwa na marafiki zake zikiwemo saa ghali ya Rolex, simu aina ya Iphone, marashi ghali miongoni mwa vitu vingine vya thamani yenye hadhi ya nyota tano.

Muigai alifurahia kupewa zawadi ya saa akifichua kuwa yake aliyokuwa akijivunia ilipotea na hakuwahi pata muda wa kuenda kununua, huku akishukuru marafiki zake kwa kugundua hilo na kuziba pengo la saa iliyopotea.

“Nilipoteza Rolex yangu miezi miwili iliyopita na sijapata kununua ingine kutokana na kuvunjika moyo kwa kuipoteza ile, kwa hiyo kupewa hii kabla nipate nguvu ya kuenda kununua tena, ni ishara kubwa inayomaanisha mambo makubwa sana kwangu,” Anerlisa alisema huku akionesha saa hiyo ya mkononi.

Pia alipakia simu ya Iphone aliyopewa na rafiki zake pamoja na marashi ya bei ghali, kitu ambacho alisema kilimkosha moyo wake pakubwa.

“Wow, ahsante wote mliofanikisha siku yangu ya kuzaliwa kwa zawadi nzuri. Shukrani zangu za dhati kutoka moyoni, Mungu awabariki nyote,” Anerlisa alionesha furaha yake.

Kupakia zawadi kutoka kwa rafiki zake kunakuja siku chache tu baada ya kuwazomea watu wanaoalikwa kwenda kwa hafla za watu na kujitoma mikono mitupu.

Anerlisa alisema kuwa mtu unapoalikwa kwenye hafla ya mtu, unafaa kuwa na uelewa kuwa ametumia muda na fedha nyingi kuandaa tafrija hiyo na hufai kuenda mikono mitupu.

Alipuuzilia mbali dhana ya kuchukua maua huku akisema kuwa maua siku zote si zawadi bali ni mapambo tu ambayo yananyauka na muda.