Ubora wako ni kutokana na marafiki 5 wa karibu, radfiki zako ni kina nani? - Kabi wa Jesus

Kabi alipakia picha ya pamoja na mkewe, Terence na mkewe, DJ Mo na mkewe na kusema hao ndio humboresha kimaisha.

Muhtasari

• Kabi alisema watu ndio chanzo kikubwa cha mafanikio ya mtu au kufeli kwake.

• "Kwa kujizunguka na mvuto mzuri mzuri tunaweza kuwa matoleo bora zaidi ya sisi wenyewe," - Kabi.

Kabi na marafiki zaake wa akribu.
Kabi na marafiki zaake wa akribu.
Image: Instagram

Katika miaka ya hivi karibuni, Sanaa ya Kenya inazidi kutanuka huku wakenya wengi wakikumbatia mifumo ya kidojitali katika kujipatia riziki. Wasanii wengi na wanablogu wamekuwa wakionesha ushirikiano wa aina yako, kinyume na awali ambapo kulikuwepo na dhana kuwa wengi ni maadui kwa sababu ya ushindani.

Kwa mwanablogu wa YouTube Kabi wa Jesus, marafiki wake wakubwa na ambao wamekuwa wakimpa msukumo wa kuzidi kufanya vizuri katika kutafuta riziki yake na mkewe ni wakuza maudhui wenzake.

Kabi alipakia picha ya pamoja akiwa na wakuza maudhui hao wengine wakiwa katika makundi ya mke na mume na kusema kwamba hao ndio marafiki wa kweli ambao wamemchochea kufanya vizuri kimaisha kwa njia chanya.

Katika picha hiyo, Mwanablogu Terence Creative na mkewe Milly Chebby pamoja na DJ Mo na mke wake Size 8 walijumuika na Kabi wa Jesus na mke wake Milly wa Jesus.

“Leo namshukuru Mungu kwa marafiki wananikusukuma kuwa bora zaidi. Je, mzunguko wako wa ushawishi una umuhimu gani? Mwisho wa siku, wewe ni matokeo ya watu 5 wa karibu unaokuzunguka. Watu ni chanzo kikubwa cha msukumo na msaada katika maisha. Kwa kujizunguka na mvuto mzuri mzuri tunaweza kuwa matoleo bora zaidi ya sisi wenyewe,” Kabi aliandika kwenye picha hiyo ya pamoja.

Siku moja iliyopita, Kabi na mkewe walitangaza kuwa huenda wanatarajia mtoto mwingine ambaye atakuwa wa tatu, miezi kadhaa baada ya kupata mtoto wa pili – binti.