Maisha ya ukapera: Harmonize arudi jikoni baada ya jiko lake kumkimbia

Msanii huyo alionekana akijiandalia vyakula mbalimbali kwa umahiri wa kipekee.

Muhtasari

• Kuonekana jikoni kunakuja wiki kadhaa baada ya kudai wahuni walimpachika mimba mjakazi wake huku pia mpenzi wake Kajala akimtoroka.

Harmonize aonesha ustadi wake jikoni
Harmonize aonesha ustadi wake jikoni
Image: Instagram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide Harmonize ameonehsa weledi na ustadi wake katika maswala ya upishi jikoni baada ya kupakia video akionesha utaratibu wa ratiba yake ya mapishi.

Msanii huyo ambaye alikuwa kitumbo wazi akiwa amevalia kaptula tu alionekana akijiandalia vyakula vyake jikoni kwa ustadi mkubwa huku akijipigia upato kuwa yeye ndiye mpishi mzuri zaidi katika maisha yake mwenyewe.

Harmonize analazimika kujiandalia chakula miezi kadhaa baada ya kudokeza kuwa wahuni walikuwa wamempachika mimba mfanyikazi wake wa ndani.

Wengi wanahisi kijakazi huyo baada ya kupata mimba, alilazimika kuondoka katika boma la kifahari la msanii huyo na hivyo huenda pengine hajapata mbadala wake na ndio maana analazimika kujifanyia shughuli za utaalamu wa tumboni.

Pia itakumbukwa kuwa Harmonize sasa hivi ni kapera huru kabisa baada ya kuachana na mchumba wake aliyemvisha pete, Kajala Masanja.

Japo hivi majuzi alionekana na mwanadada mwingine kwa jina Feza Kessy, wote wawili hawakuweka wazi iwapo walikuwa pamoja kama wapenzi au kwa ajili ya mradi wa ‘Wote’ – ngoma ambayo aliiachia mapema wiki jana na mwanadada huyo kuonekana kama vixen.

Kajala alijikata kutoka kwa lebo ya KondeGang na kuifuta kabisa taswira ya Harmonize maishani mwaka mwishoni mwa mwaka jana baada ya sekeseke za muda mrefu kuwa huenda wawili hao mambo yao yalikuwa yameingiwa na kimbunga.

Wengi walimsifia kwa kujitegemea katika suala la kujitayarishia mlo huku wakimtaka kuchukua muda zaidi kutoka kwa ulingo wa mapenzi ili kujitathmini huku baadhi wakimsuta kwa kuachana na Kajala na sasa kulazimika kuvaa viatu vya mke katika sekta ya jikoni.