Mrembo Gee atua mikononi mwa Vincent Mboya baada ya kupuruka kwa Stevo Simple Boy

Wenye midomo wanakuambia, "Ni kuoga na kurudi soko kama bado jua halijazama!"

Muhtasari

• “Huyu ni bestee wangu na tafhadhali msimwambie Stevo Simple Boy,” Mboya aliandika kwenye video hiyo ya TikTok.

Mboya aonekana na mrembo wa Stevo Simple Boy
Mboya aonekana na mrembo wa Stevo Simple Boy
Image: Tiktok, Maktaba

Wenye midomo wanasema “ni kuoga na kurudi soko” haraka iwezekanavyo.

Hii huenda ndio falsafa ambayo imemchochea mrembo Jenny Wangui ambaye wengi walimjua kwa jina Gee. Mrembo huyo baada ya kuondoka kwa msanii Stevo Simle Boy miezi kadhaa iliyopita, sasa ameibukia mikononi mwa mwanablogu wa YouTube, Vincent Mboya.

Gee na Mboya walionekana kwenye video moja yenye ukakasi ambayo mwanablogu huyo alipakia kwenye Tiktok yake na kuaisindikiza kwa maneno kuwa “mapema hushinda”

Wawili hao ambao waionekana kkatika mkao usio wa kawaida, unaochora picha kama ya kimapenzi kwenye filamu za Kifilipino Mboya alikuwa amemkumbata Gee kwa nyuma huku akiwa kama anataka kumbusu shingoni mwake.

“Huyu ni bestee wangu na tafhadhali msimwambie Stevo Simple Boy,” Mboya aliandika kwenye video hiyo ya TikTok.

Gee alijizolea umaarufu mwaka jana wakati mwanamuziki Stevo alimzindua kama mpenzi wake mpya baada ya kuachana na Pritty Vishy.

Pamoja, walionekana katika sehemu nyingi wakiwa wamevalia nguo mfanano mpaka kwa wakati mmoja kufanya video ya kuvishana pete za uchumba huku Stevo akiwaaminisha watu kuwa huyo ndiye alikuwa chaguo lake baada ya kuhangaika kushoto kulia kwa muda mrefu akitafuta mapenzi.

Baadae ilikuja kugundulika kuwa video ile iikuwa moja ya onyesho katika wimbo wake wa ‘Wedding day’ ambao alimshirikisha msanii mmoja chipukizi na siku chache baadae Gee akatangaza kuondoka kwa Stevo katika kile alisema kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi bali kuonekana kwao pamoja kulikuwa ni mradi tu wa muziki walikuwa wanafanya.

Ama kweli aliyesema Nairobi ni chumba kimoja kikubwa cha kulala kwa watu wote, anafaa kupewa heshima ya mizinga ishirini na moja!