Mwigizaji Jackie Matubia atangaza kuchukua likizo kutoka mitandaoni

Mpenzi huyo wa Blessing Lung'aho alisema akisharejea ndio atatoa sababu ya kupotea kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Muhtasari

Kusema kweli nitatoweka, kuna wakati nitatoweka kwa sababu nzuri - Matubia.

Matubia atangaza kuchukua likizo kutoka mitandao ya kijamii
Matubia atangaza kuchukua likizo kutoka mitandao ya kijamii
Image: Instagram

Mwigizaji Jackie Matubia amewatangazia mashabiki wake kuwa hivi karibuni atachukua likizo kutoka mitandao ya kijamii.

Katika ambayo walipakia kwenye YouTube yake, wakiwa na mume wake Blessing Lung’aho, Matubia alisema kuwa katika orodha ya maazimio yake mwaka huu, utafika muda hapo kati ambapo atachukua likizo ya muda lakini hakusema sababu ya kuchukua likizo hiyo.

Mwigizaji huyo maarufu alisema kuwa atakaporudi kutoka likizo hiyo ndio atawaambia wafuasi wake sababu ya kuchukua likizo huku akiwataka waendelee kumuonesha upendo kwa kuzidi kutazama kazi zake kwenye ukurasa wake wa YouTube.

"Kusema kweli nitatoweka, kuna wakati nitatoweka kwa sababu nzuri na nitawaambia kwa nini mimi na timu yangu tutatoweka," alisema na kuongeza kuwa ujio wake utakuwa mkubwa na bora.

Mumewe alifichua kuwa huenda likizo hiyo inachochewa na mradi fulani ambao alijaribu kufanya mwaka jana lakini haukupata mafanikio makubwa kam,a ambavyo walikuwa wanatarajia, jambo ambalo Matubia alikataa lakini akasisitiza kuwa sababu za kuchukua likizo hiyo ataziweka bayana baada ya kurejea.

“Utawaambia ukweli? Kwamba hufanyi hivyo kwa sababu ulijaribu na haikufanya kazi,” aliuliza, Matubia naye akajibu kwa kusema: “Mambo yakienda vizuri katika kipindi cha miezi mitatu ijayo nitafichua nilichokuwa nikipitia na nilichokuwa nacho. wamefanya ili kukamilisha.”

Matubia anaingia kweney orodha ya watu maarufu nchini Kenya ambao wamewahi tangaza kuchukua likizo kutoka mitandao ya kijamii, wengine wakisema ni kuburuzwa na kusimangwa ambako kuliwafika kwenye koo huku wengine pia wakifichua sababu mbalimbali kama kuhitaji muda wa kujitathmini na mifumo yao ya maisha mbali na mitandao ya kijamii.

Mwaka jana, mwanaharakati Bonface Mwangi aliwashangaza mashabiki wake alipotangaza kuondoka mitandaoni kwa muda ili kujjtathmini lakini baadae akarejea tena baada ya kimya cha siku kadhaa.

Wengine ambao wamewahi tangaza kuchukua likizo kutokana na sababu mbalimbali ni mwanamuziki Bahati, Nadia Mukami, mwanahabari Janet Mbugua, Lilian Muli, mwanashosholaiti Shakilla miongoni mwa wengine wengi.