Chege Chigunda atangaza kuoa miezi 3 baada ya video ya uchi wake kuvujishwa

Mwaka jana, Video ikimuonesha Chege akiwa uchi huku akipapasa uume wake ilivujishwa mitandaoni.

Muhtasari

• Chege ni mwanamuziki wa muda mrefu ambaye alitamba na kundi la TMK Wanaume Family.

Chege kuoa mwaka huu
Chege kuoa mwaka huu
Image: Instagram

Msanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva Chege Chigunda ametanaza kuwa mwaka huu wa 2023 Inshalllah atafunga ndoa.

Chege aidha alidokeza kuwa japo anatarajia ndoa lakini bado hajapata mwanadada wa kufunga ndoa naye, kwani ndoa si ya mtu mmoja bali ni wawili – mke na mume.

Aliwataka wanawake wote ambao wanajiona au kujihisi kuwa wana nafasi ya kuwa mke halali kwake kujiongeza huku akisema wanaume wanahitaji mambo machache sana kutoka kwa wanawake.

Akijitolea mfano, Chege alisema kuwa vitu anavyovitegemea kutoka kwa mwanamke wa kumuoa ni heshima, mapenzi na usikivu tu basi.

“Wanadada jiongezeni wanaume tunahitaji mambo machache sana,mfano mie Ukinipenda, Ukiniheshimu, Ukiniskiliza tu basi. Naoa mwaka huu huu 2023 chap,” Chege aliandika.

Tangazo hili linakuja mieizi mitatu tu tangu Staa huyo aliyetamba na kundi la wanamuziki la TMK kuanikwa hadharani kwenye mitandao ya kijamii baada ya video yake chafu alionekana kupiga punyeto akijirekodi huku akipapasa uume wake kuvujishwa na yule aliyesemekana kuwa mwanadada ambaye alitumiwa klipu ile.

Sekeseke hizo za mitandaoni zilisambaa kwa kasi kama moto wa jangwani huku msanii huyo akiwa amefyata ulimi na kufunga mdomo wake kwa muda huo wote wakati ambapo mashabiki wake walikuwa wanasubiria kusikia atajitetea akiwa upande gani kuhusiana na ile klipu ambayo inamuonesha kabisa mpaka uso wake pamoja na utupu wake wa mbele.

Kama wewe ni mwanadada na uliona klipu ile, maamuzi ni yako kama kujaribu bahati au kulenga tu!