Mary Wanunu awashauri mashabiki wake kufanya maamuzi sahihi 2023

Alihimiza kila mtu kufanya maamuzi sahihi 2023.

Muhtasari
  • Wanamitandao walikubaliana na mawazo yake na walikimbilia sehemu ya maoni kutoa maoni yao.
AFISA MARY WANUNU
Image: MARY WANUNU/FACEBOOK

Afisa wa polisi maarufu mary wanunu leo ​​ameamua kuwashauri watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Akichapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo alishauri kuwa watu wasipe muda, nguvu na umakini kwa mambo ambayo hayawaletei amani, faida wala malengo.

Pia alisema kuwa mambo haya yanaweza kuwa kazi ya mtu, uhusiano, ndoa, au hata biashara.

Alihimiza kila mtu kufanya maamuzi sahihi 2023.

"Ikiwa haikuletei amani, faida au kusudi, basi usiipe wakati, nguvu au umakini wako..inaweza kuwa kazi yako, uhusiano, ndoa, biashara n.k ...2023 tunafanya maamuzi sahihi,"Alishauri Wanunu.

Wanamitandao walikubaliana na mawazo yake na walikimbilia sehemu ya maoni kutoa maoni yao. 

Haya hapa baadhi ya maoni yao;

lit_mwaoo: Exactly right is the key word

Amani Amani: Morning very powerful message madam sir be blessed too

Jose's Jecy: You're absolutely right about that. No forcing issues 2023.

Kemuma Damaris: Absolutely true,,we have to make the right decision

Warren Mash: You need to give it energy n more attention for u to get profits .give more receive lessReply3 h