"Ni kuoga na kurudi soko!" Kanye West amuoa mfanyikazi wa kampuni yake ya Yeezy

Tukio hili la kinyemela linakuja miezi 2 tu baada ya kukamilika kwa talaka yake na Kim Kardashian.

Muhtasari

• Rapa huyo, 45, inasemekana alifanya sherehe ya faragha na Bianca na wawili hao wameonekana wakiwa wamevalia pete za ndoa.

• Ndoa ya Kanye na Kardashiana iliingiwa na mdudu wa vurugu mwanzoni mwa mwaka jana baada ya kudumu kwa miaka 12.

Kanye Aoa mfanyikazi wa kampuni yake ya Yeezy
Kanye Aoa mfanyikazi wa kampuni yake ya Yeezy
Image: TMZ

Miezi miwili tu baada ya mahakama kukamilisha talama ya mwanasosholaiti Kim Kardashian kutoka kwa msanii wa rap Kanye West, taarifa za chini ya zulia zinadai kuwa msanii huyo sasa ameoa tena.

Majarida ya kimataifa yanaripoti kuwa Kanye West 'amemuoa' mbunifu wa Yeezy Bianca Censori miezi miwili baada ya talaka yake na Kim Kardashian kukamilika.

Rapa huyo, 45, inasemekana alifanya sherehe ya faragha na Bianca na wawili hao wameonekana wakiwa wamevalia pete za ndoa.

Kwa mara ya kwanza Kanye alionekana akiwa amevalia bendi yake wiki iliyopita, huku vyanzo vya habari viliiambia tovuti hiyo kuwa pete hiyo inaashiria kujitolea kwake kwake kufuatia ndoa hiyo.

Licha ya kufanya sherehe ya harusi muungano huo sio halali kwa sababu wanandoa hao wanaonekana hawajaandikisha cheti cha ndoa, TMZ inaripoti.

Haijafahamika ni muda gani wawili hao wamefahamiana au wamekuwa wakichumbiana, lakini Bianca alijiunga na kampuni ya Kanye ya Yeezy mnamo Novemba 2020.

Ameorodheshwa kama Mkuu wa Usanifu na kupata nafasi hiyo baada ya kupata uzamili katika Usanifu katika Chuo Kikuu cha Melbourne nchini Australia.

TMZ ilivunja habari, Ye na Bianca walionekana wakishiriki mlo na kupiga soga huko Waldorf mapema wiki hii. Hawakuwa wameonekana pamoja kabla ya mkutano huo, lakini pia amepiga baadhi ya matukio karibu na Kanye, ikiwa ni pamoja na show ya Balenciaga mwezi Mei.