Mke wa aliyekuwa mtangazaji wa KBC, Bonnie Musambi, Betty Musambi ameandika ujumbe mzuri kusherehekea mume wake siku yake ya kuzaliwa.
Betty kwenye ukurasa wake wa Instagram alimmiminia sifa tele mtangazaji huyo wa zamani akisema alikuwa amebarikiwa kuwa naye kama mume wake.
"Heri ya kuzaliwa kwa mtu wangu wa kushangaza zaidi duniani. Mwenzangu wa maombi, baba wa ajabu kwa wasichana wetu wawili warembo, rafiki yangu mkubwa, Mkurugenzi Mtendaji wangu...nitamsifu Mungu daima kwa kutufanya wenzi wa ndoa. Uhusiano wetu hauwezi kuvunjika na kwa hilo nimebarikiwa sana. Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu,” Betty aliandika.
Bonnie Musambi katika kuenzi siku yake ya kuzaliwa alisema amebarikiwa kuwa na afya njema jambo ambalo hakulichukulia kawaida.
Musambi alifichua kwamba siku yake ya kuzaliwa ni ya kipekee kwani hakuzaliwa baada ya miezi tisa ya kawaida na hata ana jina la kipekee kwa hilo.
“Halo Watu Wote 👋, Kula, kunywa na kufurahi kwa sababu ni siku yangu ya kuzaliwa!😊😊😊 Kwa namna fulani, unajua kuzaliwa kwangu kulikuwa na utata kidogo? Nilizaliwa Ijumaa tarehe 16 Januari, 9.30pm, BAADA YA MIEZI KUMI NA MOJA (Siyo tisa). Baba yangu aliniita MUTISYA, kwa kuchelewesha hedhi ya kawaida ya kuzaliwa. Kisha akatabiri kwamba siku zote nitafanikiwa mambo makubwa katika ulimwengu huu (Amina kwa hilo). Ninampa Mungu Utukufu wote kwa kunitunza muda wote huu; kwa dhati siichukulii poa. Pia ninaishukuru familia yangu kwa upendo na utunzaji wa ajabu,” Musambi alisimulia.
Musambi ambaye kwa sasa ni mjasiriamali katika tasnia ya habari na mawasiliano anaendesha kituo chake cha redio kinachopeperusha matangazo kwa lugha ya Akamba.