Georgina Njenga arejea mitandaoni kwa kishindo baada ya picha zake chafu kuvujishwa

“Njia pekee ya kunishinda ni iwapo nitakufa moyo,” Georgina Njenga aliandika.

Muhtasari

• Georgina alikubali kuwa picha hizo zilikuwa zake lakini akasema kuwa ni za kipindi akiwa tineja wa miaka 17.

Mpenzi wa Baha, Georgina Njenga arejea mitandaoni
Mpenzi wa Baha, Georgina Njenga arejea mitandaoni
Image: INSTAGRAM

Georgina Njenga, mpenzi wa mwigizaji Baha Mchachari amerejea mitandoni kwa vishindo vya aina yake, wiki mbili baada ya video ya utupu wake kuvujishwa mitandaoni na mtu ambaye hajajulikana.

Njenga alipakia picha moja akiwa ameketi na kuachia ujumbe wa kishindi unaolenga kuwatia kiwewe mahasidi wake akiwaambia kuwa kama walikuwa wnafikiria kumchafua kwa kumdhalilisha basi wamepiga simu kwa namba mbaya.

Aliwaambia kuwa njia pekee ya kumpiku au kumshinda katika mishemishe zake ni iwapo ataacha kufanya anachokifanya, jambo ambalo alidokeza kuwa hayuko karibu na kukoma kujisukuma kimaisha.

“Njia pekee ya kunishinda ni iwapo nitakufa moyo,” Georgina Njenga aliandika.

Wiki mbili zilizopita mama huyo wa mtoto mmoja alidhalilika hadi kushindwa pa kuficha sura yake baada ya mtu kuvujisha video akiwa uchi huku akisakata densi, video ambazo ziliwaunganisha Wakenya mitandaoni kwa zaidi ya saa 24.

Baha na Georina waligeuka gumzo la kuzungumziwa kwenye mtandao wa Twitter na Baha katika mahojiano na kituo kimoja cha habari, alisema kuwa hakuwa tayari kumuacha Georgina kwa gharama yoyote ile huku pia akiapa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu aliyezivujisha picha za mpenzi wake akiwa katika suti ya Mungu.

"Mipango inaendelea, tutachukua hatua za kisheria," alisema.

Hapo awali, Bi Georgina alikuwa amedai kwamba mpenzi wake wa zamani ndiye aliyehusika katika uvujishaji wa video hizo chafu.

Alisema kuwa video hizo hazikuwa za wakati huu bali ni za kipindi akiwa tineja wa miaka 17 ndio mpenzi huyo wa zamani alizichukua na hakuwa anajua kama angezihifadhi.