Milly Chebby asimulia jinsi kuchelewa kwa hedhi yake kulimpa wasiwasi wa mimba

"Zilichelewa na hadi nikasema niko tayari kwa safari ya mimba na malezi,” Milly alisema.

Muhtasari

• Mwanablogu huyo alisema alichangaanyikiwa baada ya hedhi yake kuchelewa huku akishuku kuwa huenda mpango wa uzazi umefeli.

Milly Chebby asimulia woga wa mimba
Milly Chebby asimulia woga wa mimba
Image: Instagram

Mwanablogu Milly Chebby kwa mara ya kwanza amezungumzia jinsi aliingiwa na woga wa kupata mimba baada ya siku zake za hedhi kupita bila kupata hedhi zake.

Kupitia instastories zake, Milly Chebby alipakia video akisimulia wasiwasi wake mwezi wa Desemba ambapo alifikiri amepata mimba pasi na kujipanga.

Milly alisema kuwa pengine ni homoni za mwili wake zilipishana kidogo kutokana na hali ya anga katika mazingira ambayo alikuwa anatembelea kipindi cha sherehe za sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

Alisema kuwa alikwenda Nigeria ambapo hali ya anga ilikuwa ni joto kali kabla ya kurudi Nairobi ambapo hali ilikuwa tofauti na Baridi kali, jambo ambal alisema huenda ndilo lilichangia kupotea kwa hedhi yake kwa muda.

“Desemba nilibadilisha mazingira kwa mara kadhaa, nilikuwa Lagos ambapo kulikuwa na joto kali, nikarudi Nairobi ambapo kulikuwa na baridi kali na kisha kuenda Naivasha ambapo pia hali ilikuwa ya kijibaridi. Na nafikiri mwili wangu ulishtuka sana na kwa mara ya kwanza tangu nibakeghe, sikupata hedhi yangu hadi nikajishuku nina mimba. Zilichelewa na hadi nikasema niko tayari kwa safari ya mimba na malezi,” Milly alisema.

Mwanablogu huyo alisema alichangaanyikiwa baada ya hedhi yake kuchelewa huku akishuku kuwa huenda mpango wa uzazi umefeli.

Baadae ziliporudi, Milly Chebby alisema kuwa alifurahia na kusema kuwa mzungumzo huo wa kuanza kulea mimba hadi mtoto alikuwa ameanza kuukubali kichwani mwake lakini sasa amefuta fikira hizo ambazo zilikuwa zimemtia mashaka.