Shakilla: Mbona sipati mwanamume wa kunitongoza? Au nilikusudiwa kuwa singo maishani?

Mwishoni mwa mwaka jana, Mwanasosholaiti huyo alidokeza kuwa huenda mwaka huu akaonekana akiigiza filamu za watu wazima.

Muhtasari

• "Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” - Shakilla.

• Shakilla alishangaa kuwa licha ya umaarufu na ufuasi mkubwa Instagram, hakuna mwanaume anayejaribu kumpenda.

Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Shakilla ameonesha wasiwasi wake jinsi wanaume wote wamemkwepa na hakuna anayetaka kuanzisha uhusiani naye au haya kumtongoza.

Kupitia Instagram yake, Shakilla alidhihirisha mashaka yake kwa kujiuliza maswali mengi ya balagha kuhusu ni kwa nini hakuna mwanaume hata mmoja kutoka kwa wafuasi wake zaidi ya laki tatu kwenye mtandao huo hawataki kujihusisha naye kimapenzi

Pia alijikuna kichwa kwa swali la iwapo yeye aliumbwa kuwa wa mitaani na si mtu wa kuchumbiwa na kupelekwa nyumbani kujenga boma kama mwanafamilia.

“Kwa hiyo tuseme katika wanaume wote ambao wananifuata Instagram hakuna hata mmoja anayetaka kuingia katika uhusiano wa hakika na mimi. Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” Mwanasosholaiti huyo aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

Shakilla ambaye umaarufu wake ulichibuka kutokana na kipindi cha mtangazaji Xtian Dela wakati janga la Korona lilipobisha nchini, wiki kadhaa zilizopita alimwanika mwanablogu Andrew Kibe kwa kuonesha jinsi aliingia kwenye DM yake faraghani na kujaribu kumtongoza.

Wengi wanahisi huenda wanaume wamemuogopa kutokana na tabia hiyo ya kutoweka siri kile kinachoendelea katika DM zake, huku wakisema kuwa huenda wkijaribu kumtongoza atavujisha mazungumzo yote na mwisho wa siku kuwadhalilisha wanaume.

Katika siku za hivi karibuni, Shakilla ameonekana kuwa na usumbufu mwingi wa kiakili huku kwa wkati mmoja pia akikubali kuwa huenda ana msongo wa mawazo na tatizo la unyongovu.

Mwishoni mwa mwaka jana, alifichua kuwa huenda mashabiki wake mwaka huu wakamuona anajaribu kutafuta riziki kwa njia tofauti kabisa kwenye kuigiza filamu ya watu wazima.