Mwigizaji Selina amsifia mwigizaji mwenzake Kate Actress

Mwigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress amekuwa kwenye tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 5

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wa mwigizaji Celestine Gachui almaarufu Selina amemlimbikizia sifa Kate, huku akisema amekuwa mfano mwema kwenye tasnia ya uigizaji
MWIGIZAJI CELESTINE GACHUI NA MWIGIZAJI CATHERINE KAMAU
Image: HISANI

Katika tasnia ya burudani sio wasanii au waigizaji wote ambao huwatakia wenzao maisha mema au kuwalimbikizia sifa kila wanapopata nafasi.

Asilimia kubwa ya wasanii wamekuwa wakifokeana na kushambuliana mitandaoni jambo ambalo mashabiki wao wamekuwa wakisema ni shoo mbaya kwao.

Mwigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress amekuwa kwenye tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 5,huku akifahamika sana kupitia kwa bidii ya kazi yake ya uigizaji.

Kupitia kwenye ukurasa wa mwigizaji Celestine Gachui almaarufu Selina amemlimbikizia sifa Kate, huku akisema amekuwa mfano mwema kwenye tasnia ya uigizaji.

Aidha aliongeza kwamba akimuona Kate huwa anaona mambo makubwa kwani amekuwa motisha wake.

"Leo ninamsherehekea mwanamke huyu @kate_actress , ndiye motisha yangu 🥰 haswa kwenye tasnia yetu hii. Ninapomwona naona mbali zaidi💃❤,"Aliandika Selina.