Nyinyi wote ni wachafu, hamuwezi faulu kimuziki - Mwijaku awafokea Harmonize na Rayvanny

"Mna mapungufu mengi ila jamii iliamua kukaa kimya. Kwa hiki mnachokifanya ni upumbavu,” - Mwijaku.

Muhtasari

• Harmonize na Rayvanny walichafuana vikali kwenye instagram usiku wa kuamkia Jumanne, kila mmoja akimchafua mwenzake kwa kashfa za nguoni.

Mwijaku awafokea Harmonzie na Rayvanny
Mwijaku awafokea Harmonzie na Rayvanny
Image: maktaba

Mwijaku amewakoromea wasanii Harmonize na Rayvanny katika ugomvi wao kupitia Instastories ambapo walishambuliana vikali na kuanikana kwa mashabiki wao kwa kutupiana maneno ya nguoni.

Ugomvi wa wawili hao ulianza pale Harmonize aliandika kuwashauri wasanii kutotoa ngoma zinazozungumzia pombe, akilenga wimbo wa Rayvanny akimshirikisha bosi wao wa zamani Diamond Platnumz.

Hapo ndipo Rayvanny alicharuka kama simba bukaa aliyejeruhiwa na kuasha moto mkali ambao Harmonize naye kwa upande mwingine alijaribu kuuzima.Mwijaku ambaye alikuwa anafuatilia ugomvi huu wa kuanikana aliwasuta wote na kusema ni wapumbavu ambao jamii imevumilia licha ya mapungufu yao.

Mtangazaji huyo alisema kuwa kati ya hao wawili, hakuna aliye msafi kwani wote ni wachafu na jamii ina siri zao nyingi na haijazivujisha lakini wao wametofautiana kidogo tu na tayari wameupiga mwingi, kuzungumzia mpaka yale ambayo hakuna mtu alikuwa anataka kuyasikia.

“Mmedhihirisha udogo wenu katika Sanaa, kwa tabia hizi mlizo nazo kamwe hamuwezi kuendelea kisana. Mtabaki mkitogana tu. Kama hamjui jamii inajua kuwa nyinyi wote ni wachafu. Na mna mapungufu mengi ila jamii iliamua kukaa kimya. Kwa hiki mnachokifanya ni upumbavu,” Mwijaku alifoka.

Katika kutupiana maneno, wawili hao walivuka mipaka na kutaja mihela kila mmoja alilipa ili kuruhusiwa kuondoka Wasafi ya Diamond, huku Vanny Boy akisema alilazimika kuzama mfukoni na kutengana na kiasi cha bilioni 1.3 pesa za Tanzania.

Kwa upande wake, Harmonize alitoa kima cha milioni 600 ili kuvunja mkataba wake na Wasafi.