Cartoon Comedian: Ningependa kushiriki mapenzi katika ofisi ya binti wa kwanza wa taifa

Mchekeshaji huyo katika wimbo wake alisema angependa kutoka kimapenzi na rapa Nyashinski.

Muhtasari

• Wimbo huo mpaka sasa una watazamaji zaidi ya elfu hamsini kwenye mtandao wa YouTube.

Mchekeshaji Cartoon Comedian asemqa alisalitiwa kimapenzi
Mchekeshaji Cartoon Comedian asemqa alisalitiwa kimapenzi
Image: Instagram

Vanessa Akinyi, ambaye wengi wanamjua kama mchekeshaji Cartoon Comedian ameacha mitandao ya kijamii katika cheche kali baada ya kuachia wimbo akionesha wazi kutamani kutoka kimapenzi na msanii Nyashinski.

Katika wimbo wake mpya alioutoa wikendi iliyopita wenye mada ‘Enough’ Cartoon alisikika kwenye vesi ya kwanza akikiri hadharani kuwa kama kuna kitu lazima tu akifanya maishani mwake ni kutoka kimapenzi na rapa huyo wa muda mrefu.

Katika wimbo wa rap, mwanamuziki huyo wa kuchekesha hakushiriki tu kupendezwa kwake na Nyashinski bali pia aliwarushia vijembe wanaomchukia huku akijaribu kusimame dhidi ya watu wanaomsaliti.

“Doh na make ni ya kutosha. Na chali anaipiga ako fiti, si ati nini. Sijakua mrembo kabisa, akili nilipewa imetosha. Sijawai amini kuna mapenzi, cheki napenda d**k kama upuuzi. Maskini asiwai Ku advice he'll never make sense. Chuki pelekea mamako. Kuna vitu lazma ni do. Kama kuf**k the goat Nyashinski.” Sehemu ya wimbo huo wenye maneno makali yenye kashfa uliimba.

Mchekeshaji huyo alizidi kugongelea misumari mikali kwa kusema kuwa ana ndoto ya kushiriki mapenzi katika ofisi ya binti wa kwanza wa taifa, Charlene Ruto.

Wimbo huo mpaka sasa una watazamaji zaidi ya elfu hamsini kwenye mtandao wa YouTube.

Kabla ya kuachia wimbo wake mpya zaidi, Cartoon, Oktoba 2022, alitoa wimbo mwingine uliopewa jina la ‘Mbona Unacheat’, ambamo alionyesha kutofurahishwa kwake na hisia zake kwa mpenzi wake wa zamani, ambaye waliachana naye kwa tabu.

Septemba 24, mchekeshaji huyo alisema katika ukurasa wake wa Instagram kwamba alikuwa akiumia sana baada ya kuachana na mpenzi wake huyo kwa ujumbe aliouweka ‘Mbona Unacheat’ ambao uligeuka kuwa jina la wimbo huo mpya.