logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Samidoh amjibu DP Gachagua kwa kauli ya kudhibiti wake zake Edday na Nyamu

Gachagua alimtaka Samidoh kuchukua jukumu la kuleta maelewano kati ya wake zake.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri24 January 2023 - 12:29

Muhtasari


• Nyamu na Edday walipapurana vikali mwishoni mwa mwaka jana katika shoo ya msanii huyo huko Dubai.

• Gachagua alitaja tukio hilo kama la kuleta aibu kwa kuonesha mienendo yao kwa nchi ya watu.

Samidoh amjibu Gachagua

Baada ya naibu wa rais Rigathi Gachagua kumtaka Samidoh kuchukua jukumu la kuwamudu wake zake wawili Edday Nderitu na Karen Nyamu la sivyo watamchukulia hatua, sasa mwanamuziki huyo ametoa matamshi yanayolenga kumjibu naibu rais.

Jumatatu katika hafla ya mazishi ya dadake waziri Moses Kuria, Gachagua alipanda jukwaani na kuzungumza kwa utani akimwambia Samidoh moja kwa moja usoni kuwa ni aibu aliyoionesha huko Dubai wakati wake zake walipapurana hadharani jukwaani.

Gachagua alimwambia kuwa ni wakati sasa awadhibiti wote ili kama ni kupigana wafanya hivyo wakiwa humu nchini wala si kuonesha tabia zao kwa watu wan je kuenda kupigana nje ya nchi.

Naibu rais alimshauri afisa huyo wa polisi kufanya hima ili kufanikisha hilo kwani hakuna ndovu anayeshindwa kubeba pembe zake, huku akisema kuwa akishindwa basi watamuadhibu kwa sababu ni afisa wa polisi.

“Samidoh wewe ni rafiki yangu Lakini kuna mahali unatuangusha kidogo, sasa wewe Samidoh udhibitil hiawa watu wako, Hakuna tembo ambaye hana uwezo wa kubeba majukumu yake. Unachofanya Samidoh, unasafiri peke yako ili tusiwe na aibu huko ughaibuni. Ukienda kusababisha maigizo huko wanatuzoea na hatutaki masuala yetu yameisha. Ikiwa huwezi kudhibiti hilo bado wewe ni afisa wetu, tutakunyima visa na kukuadhibu,” naibu rais alimwambia.

Samidoh alionekana kujutia kilichotokea Dubai na kunukuu maneno ya waziri Moses Kuria akisema kuwa hakuna msafi ambaye hana nyakati zake chafu za nyuma, na pia hakuna mchafu ambaye hana nafasi safi katika siku za usoni.

“Hakuna malaika msafi ambaye hana nyakati zake za nyuma chafu, na hakuna mchsfu mwenye dhambi ambaye hana nafasi katika siku za usoni,” Samidoh alinukuu maneno ambayo alisema yalitamkwa na waziri wa viwanda na biashara Moses Kuria.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved