Anahitaji huruma- Karen Nyamu amjibu Samidoh baada ya kumwita chura

Mmoja wa wafuasi wake alitoa maoni akisema kuwa anaonekana mrembo hata kama mtu angemwita chura.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wa facebook wa Karen alichapisha ujumbe ambapo alisema kwamba hakuwa peke yake tangu wakati wote na kila msimu Mungu alitembea pamoja naye
Nyamu asema haachi pombe
Nyamu asema haachi pombe
Image: Facebook

Siku chache zilizopita Samidoh na Karen Nyamu walishambuliana mitandaoni  na kuwaacha wanamitandao na hisia mseto.

Baada ya Karen kuanzisha pambano hilo na kumwita Samidoh kuwa ni mtu ambaye hajatahiriwa, Samidoh alishindwa kuzuia hasira ambapo aliamua kumrushia Nyamu cheche za maneno.

Samidoh alisema kuwa hata iweje hawezi kupeleka chura kwa mama yake ili kuwafurahisha watu ambapo alikuwa akimtaja Karen Nyamu kama mjeledi.

Kupitia kwenye ukurasa wa facebook wa Karen alichapisha ujumbe ambapo alisema kwamba hakuwa peke yake tangu wakati wote na kila msimu Mungu alitembea pamoja naye.

Mmoja wa wafuasi wake alitoa maoni akisema kuwa anaonekana mrembo hata kama mtu angemwita chura.

"Huyo ni msichana wangu, unakaa mrembo wakitutukana chura tunaruka ruka mbele,"Aliandika shabiki.

Karen alijibu hili akisema mwanamume anapofikia hatua hiyo ya kumtusi mwanamke anahitaji huruma na watu wasimhukumu.

Aliendelea na kusema kama angejua kuwa chura hamhitaji tena angekuwa tayari amefuta maoni hayo.

"Mwanaume akifika hio point anahitaji huruma dont judge him. Kwanza akikumbuka hio chura ata haina kazi yake inabidi adelete tu hio comment😂😂,"Aliandika Karen.

Wawili hao waliachana mwaka jana baada ya kusababisha drama Dubai.