DJ Evolve kuzindua hazina ya kuwasaidia walemavu

Katika taarifa amesema hazina hiyo itawahusisha watu wanaoishi mashinani na kimataifa.

Muhtasari
  • Tamasha hizo zimepangwa kufanyika kila mwezi jijini Nairobi na kote nchini, na mapato kutoka kwa tukio litaelekezwa katika The Evolve Fund
DJ Evolve na Juliani
DJ Evolve na Juliani
Image: INSTAGRAM

Mcheza santuri Felix Orinda anayejulikana pia kama DJ Evolve ametangaza mpango wake wa kuanzisha hazina ya  kusaidia watu wanaoishi na ulemavu.

Katika taarifa amesema hazina hiyo itawahusisha watu wanaoishi mashinani na kimataifa.

Katika taarifa yake, DJ Evolve alisema kupata nafasi ya pili, nafasi ya maisha kufuatia mkasa uliomsababishia ulemavu ilimtia moyo kuanzisha hazina ya The Evolve kusaidia watu wenye ulemavu nchini Kenya na kimataifa.

Tamasha hizo zimepangwa kufanyika kila mwezi jijini Nairobi na kote nchini, na mapato kutoka kwa tukio litaelekezwa katika The Evolve Fund

Tamasha la kwanza linatarajiwa kufanyika Februari 12, 2023, na miongoni mwa wacheza santuri ambao tayari wamethibitishwa kuhudhuria tukio hilo ni pamoja na DJ Purpl,DJ Saint Kevinsky,DJ Mjay Kenya,DJ Namosky,DJ Twinn 48 miongoni mwa wacheza santuri wengine.

Ili kuchangisha fedha, DJ Evolve alishirikiana na Tufund, jukwaa la ufadhili wa watu wengi ambalo hutafuta kuwezesha watu kupata ufadhili kwa sababu tofauti, na Matukio ya Mtickets kuandaa matukio ya matamasha yaliyopewa jina la Evolution.