Willis Raburu:Daktari alisema singeweza kupita Desemba 2022

Raburu anasema ni wakati umefika watu waache kuwadharau wengine.

Muhtasari
  • Katika mahojiano na BBC News Africa, Raburu anasema kuwa ilimsukuma kufanya mabadiliko katika mtindo wake wa maisha
Willis Raburu katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mwanahabari Willis Raburu amefichua kuwa madaktari walikuwa wamempa ratiba, wakisema angekuwa amefariki  kufikia Desemba 2022.

Hii ilitokana na  uzito wake kupita kiasi ambao ulifanya mishipa yake kuanza kupungua.

Katika mahojiano na BBC News Africa, Raburu anasema kuwa ilimsukuma kufanya mabadiliko katika mtindo wake wa maisha.

"Daktari alisema nisingeliweza kupita Desemba 2022. Nilipofiwa na binti yangu, nilikula sana Nilikuwa nikila kila kitu na kwa kiasi kikubwa. Kunywa pombe.Siku niliyoenda kupima nilikuwa na kilo 164 na sikuamini

Daktari aliniambia kutokana na jinsi moyo wangu ulivyokuwa unatenda nilikuwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu.Aliniambia kufikia Krismasi ningepatwa na kiharusi, mshtuko wa moyo au kitu kingine,"Rabiuru alisimulia.

Raburu anasema ni wakati umefika watu waache kuwadharau wengine.

Hapo awali alijaribu kufanya mazoezi, kuondoa sumu mwilini na njia nyingine nyingi za kupunguza uzito bila mafanikio.

Ndiyo maana anachagua kuwa na njia ya 'gastric by-pass'

"kukejeli mtu kwa ajili ya uzito wa mwili wake si haki kwa sababu mimi huamka na kulala katika mwili huu.Nazunguka ndani yake. Unafikiriaje unaponiambia kile ninachojua tayari?"