Wiki chache zilizopita Karen Nyamu alitangaza hadharani kumalizika kwa uhusiano wake na Samidoh baada ya drama ya Dubai ambapo alikabiliwa na mke wa Samidoh Eddy Nderitu.
Siku ya Jumanne Karen alikuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Redio humu nchini ambapo alizungumzia kisanga cha Dubai na Samidoh.
Karen alimtambua msanii huyo wa Mugithi kama baba anayewajibika kwa watoto wao.
Alisema wakati wa drama ya Dubai alikuwa amekunywa pombe kali ambayo hajawahitumia na ilimfanya asababishe drama hiyo.
Pia aliweka wazi kuwa kwa sasa yuko single na hayuko tayari kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi hivi karibuni.
Aliongeza kuwa Samidoh ni mwanamume anayewajibika sana na baba mzuri kwa watoto wao akisema ingawa Samidoh huwa anamwangusha hajawahi kuwaangusha watoto wake na yuko kwa ajili yao kila wakati.
Alitoa mfano mmoja akisema kwamba mtoto wao wa kwanza alipokuwa akijiunga na shule licha ya kumpuuza, aliendelea na kumpelekea karo.
Kisanga cha wawili hao kilizua hisia mseto mitandaoni, huku naibu Rais Gachagua akimtumia msanii huyo onyo na kumwambia anapaswa kuwathibiti watu wake ili kupunguza aibu kwa mashabiki wake na Wakenya kwa jumla.