Waunda maudhui Terence creative na mkewe Milly Chebby, kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, wamemwandikia bnti yao ujumbe mtamu,huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Terence na mkewe wanafahamika sana mitandaoni kwa kuweka tabasamu kwa mashabiki wao.
Milly alimtakia bintiye heri njema ya siku ya kuzaliwa huku akimwambia kuwa huwa anajaza moyo wake kwa upendo tele.
"Katika siku yako ya nne ya kuzaliwa mtoto wangu wa ajabu @millanetai , ninakutakia siku zijazo zenye afya njema zilizojaa upendo na furaha, mpenzi wangu! Natumai siku yako maalum imejaa furaha na furaha! Heri ya miaka 4 ya kuzaliwa kwa binti yangu mdogo mpendwa! Unaujaza moyo wangu kwa upendo mwingi, na kila siku najiambia jinsi nilivyobarikiwa kuwa na binti kama wewe!"
Terence kwa upande mwingine alisema;
Kwa mwigizaji kitinda mimba wangu,heri njema ya siku yako ya kuzaliwa malkia wangu nakupenda sana @millanetai ❤️❤️❤️❤️❤️Mungu akubariki mwaka huu mpya furahiaToto,"Terence alisema.
Mahabiki walimtakia mwanawe Terence na Milly heri njema ya siku ya kuzaliwa na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;
Flaqo411: Happy birthday to Milla❤️❤️🙌🙌
turk_voices: Ni kama Ako acting Kwa muda mfupi sana 😂. Happy Birthday Milla 😍
wamarich: God grant her knowledge to Excell in life and have many more birthdays 🥳🎉
naturalhairkenya: Aww she's so big now! How time flies! Happy birthday beautiful princess 🎂🥳🥰 may God always protect you and favor you 💓
bettychels: Happiest birthday little champ God continue to protect and guide you throughout your life lots of love ❤️❤️