Diamond Platnumz amsaini msanii mpya kwenye lebo ya WCB Wasafi

Diamond alitangaza hilo kwenye Instagram yake japo hakuweka wazi jina la msanii wake mpya.

Muhtasari

• Sajili hiyo mpya inaziba pengo lililoachwa na Rayvanny aliyeondoka mwaka jana baada ya miaka 6 kwenye lebo hiyo.

Diamond atangaza kuzindua msanii mpya Wasafi
Diamond atangaza kuzindua msanii mpya Wasafi
Image: Instagram

Msanii Diamond Pltnumz ambaye ndiye mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Wasafi inayojumuisha vituo vya habari – redio na runinga pamoja na lebo ya muziki wa WCB Wasafi ametangaza kumsaini msanii mpya kweney lebo hiyo.

Kupitia baruac ya mkataba ambayo Diamond alipakia kwenye Instagram yake, ianonesha kwamba kuna msanii mpya ambaye amejiunga na lebo yake ya Wasafi japo hakutoa taarifa ziaidi kuhusu hilo.

“Tarehe Mbili mwezi wa pili mwaka 2023, siku nyingine yenye Baraka kwa msanii mchanga mwenye Baraka,” Diamond aliandika kwenye picha hiyo ya barua ya mkataba.

Barua hiyo ilikuwa na mada ya, “Mkataba wa kujiunga na kampuni ya Muziki” huku ukitoa maelezo kwamab unaanza kufanya kazi Februari tarehe 2, ukiwa ni mkataba kati ya;

“Wasafi Limited (LTD) kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania kufanya shughuli za Sanaa yenye makao yake makuu Kijitonyama…” sehemu ya barua hiyo ilisoma huku ikitoa anwani lakini ilificha maelezo zaidi.

Kusainiwa kwa msanii mpya kunakuja wiki chache tu baada ya uvumi kuibuka kwamba Marioo alimfuata Diamond akitaka kusainiwa ili kufanya kazi chini ya lebo ya Wasafi.

Diamond alimwaga mtama huu katika mahojiano ya kipekee na Wasafi lakini Marioo mwenyewe alijitokeza na kukana madai hayo akisema kwamba Diamond aliteleza tu ulimi wala hakukuwa na ukweli wowote kuwa alitaka kusainiwa Wasafi.

Tangu kuondoka kwa Rayvanny, WCB Wasafi imebaki na wasanii watatu tu ambao ni Zuchu,, Mbosso na Lavalava ambaye miziki yake kwa miaka ya hivi karibuni haijakuwa ikisikika vile kama ambavyo ilikuwa inasikika siku za nyuma akiwa kipya kinyemi Wasafi.

Harmonize alikuwa wa kwanza kuvunja mkataba wake kutoka Wasafi mwaka 2019  na kuanzisha lebo yake mwenyewe ya Konde Music Worldwide huku Rayvanny akimfuata miaka 3 baadae ambapo pia alifungua lebo yake kwa jina Next Level Music.