Mpelelezi Jane Mugoh kufanya 'postmortem' kubaini kilichoua mbwa wake

"Umeacha watoto watatu wakiwa na umri wa wiki mbili. Hatutasahau bora zaidi uliyotoa" - Mugoh aliomboleza.

Muhtasari

• Mugoh alisema kuwa mbwa huyo aliwaacha watoto watatu wa wiki mbili na kupitia kwao atazidi kumkumbuka milele.

Jane Mugoh aomboleza kifo cha mbwa wake
Jane Mugoh aomboleza kifo cha mbwa wake
Image: facebook

Mpelelezi wa binafsi Jane Mugoh anaendelea kuomboleza kifo cha mmoja wa mbwa wake wakali katika kampuni yake ya binafsi ya upelelezi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mugoh alihadithia wasifu wa mbwa huyo aliyekufa kwa njia tata, huku akisema kuwa ni mtoto wa mbwa maarufu kwa jina Hitler aliyeonekana naye kwenye video ya Makala ya BBC mwaka 2020.

Alisema kuwa kifo cha mbwa wake bado hakijamuingia kichwani na hivyo atalazimika kufanya uchunguzi wa maiti ili kubaini kilichosababisha kifo chake.

Mugoh alisema anapenda mbwa hata kama watu wanamshangaa ni kwa nini anapenda mbwa na kusema kuwa uaminifu utokanao kwa mbwa ni adimu sana kupatikana kwa biandamu yeyote.

“#Rip Tango mwana wa kwanza wa Hitler mbwa aliyevuma Ulimwenguni kote 2020. Ulikuwa mbwa mtiifu zaidi katika familia yetu. Uchunguzi wa maiti utakagua kile kilichokuuwa jana usiku 😭😭.”

“Watu huniuliza kwa nini ninawapenda mbwa. Ni nadra sana kupata aina ya uaminifu kutoka kwa wanadamu unaopata kwa mbwa. Mbwa atakaa kwenye kaburi lako akiomboleza na kulia akitokwa na machozi, wakati mume wako, mke, rafiki wa kike, bosi, mfanyakazi au mpenzi wako amehamia familia inayofuata mara tu unapokufa,” Mugoh alisema.

Mugoh alisema kuwa mbwa huyo aliwaacha watoto watatu wa wiki mbili na kupitia kwao atazidi kumkumbuka milele.

“Tulikupenda Tango.Umeacha watoto watatu wakiwa na umri wa wiki mbili. Hatutasahau bora zaidi uliyotoa.Rip.Itatunza watoto wako wa mbwa,” aliomboleza.

Mpelelezi huyo alichukua fursa hiyo kuelezea umuhimu wa mbwa akisema kwamba ndiye rafiki pekee wa kikweli asiyeweza kukuacha wakati wa dhiki na faraja.

“Unaweza kuwa unahisi huzuni, na hakuna mtu anayeweza kutambua. Lakini mbwa wako ataona na kujaribu kukupa moyo. Na uzuri wa hilo ni kwamba hawana ajenda. Angalia watu wasio na makazi. Familia zao zinaweza kuwaacha, lakini mbwa wao hawatawaacha kamwe,” alisema.