logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakati wa Mungu-Msanii wa Tanzania Ray C asema huku akitangaza anatarajia mtoto

Hata hivyo alipoelekeza kamera kwenye eneo la tumbo lake

image
na Radio Jambo

Yanayojiri06 February 2023 - 15:23

Muhtasari


  • Ray C, ambaye ana umri wa miaka 40 sasa, aliandamana zaidi na chapisho hilo na nukuu inayosema juu ya ujauzito wake

Mwimbaji mashuhuri wa Tanzania Rehema Chalamila maarufu kama Ray C anatarajia mtoto.

Mwanamuziki huyo ambaye ni mshindi wa tuzo amebainisha hayo leo kupitia akaunti yake ya Instagram, ambapo alichapisha kipande kifupi cha video kilichoonyesha kuwa alikuwana ujauzito.

Hata hivyo alipoelekeza kamera kwenye eneo la tumbo lake, ilionekana wazi kuwa msanii huyo wa 'Sogea Sogea' alikuwa na ujauzito.

Ray C, ambaye ana umri wa miaka 40 sasa, aliandamana zaidi na chapisho hilo na nukuu inayosema juu ya ujauzito wake, akisema kuwa wakati wa Mungu ulikuwa bora zaidi.

"Wakati wa Mungu ni wakati sahihi.🙏🏾🙏🏾❤️,"Aliandika Ray C.

Wanamitandao walichukua fursa hiyo na kumpongeza mwanamuziki huyo, na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

kajalafrida: Jamani hongera sana baby ❤️❤️❤️

talliaoyando: Congratulations love ❤️

rosa_ree: Alilililililiiiiiiii 🎉 congrats my loveeee😆 so excited for you! Mungu akutangulie ❤️

officialshilole: Woyooooooooooooo mashaaallhaaa sis😍

the_ironlady1976: Hongera my Ninjaaa👏👏👏 Mungu azidi kukubariki .Yesu azidi kukulinda Angalia Mungu alivyo mkubwa Usikate tamaa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved