Fomu ni nywele fupi: Millicent Omanga ajitapa na mtindo mpya wa nywele

Omanga anaungana na wanasiasa wengine kama Aisha Jumwa, Sabina Chege na wengine katika mtindo huo.

Muhtasari

• Mtindo huo uliwasisimua wafuasi wake ambao walimhongera na kumtaka aendelee nao.

Millicent Omanga atokea na muonekano mpya
Millicent Omanga atokea na muonekano mpya
Image: Facebook

Aliyekuwa seneta maalum Millicent Omanga ameibuka na mtindo mpya wa nywele ambao umewasisimua mashabiki na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Omanga ambaye wengi wamemzoea kuwa na mtindo wa kusuka nywele, safari hii aliamua kujaribu kitu kipya na kutokea na mtindo wa nywele fupi.

Aliwauliza mashabiki wake kuweka alama ya ndio au la, akisema kuwa chochote ambacho wangesema ndicho angekifanyia kazi – kwa maana kwamba kama walipenda mtindo wake wa nywele fupi basi ataendelea kutokea hivyo na kama wangekataa basi angerudi kwa mtindo wa kusuka.

“Rada iko aje hapa? Vile mtasema ndivyo nitafanya,” Omanga aliandika.

Wafuasi wake kwenye mtandao wa Facebook wengi walionekana kufurahishwa na mtindo huo wake wakisema ulimfanya akawa mbichi hata Zaidi.

“Lo! Swali kuu ni kwa nini hii inachukua muda mrefu sana kutokea katika ukweli? Hayo yanaweza kuwa mabadiliko mazuri. Napenda sura mpya kama hii. Hii itakuwa dhahiri mwenendo,” Stacey Waweru alimwambia.

Hata hivyo, kuna baadhi waliokosoa mtindo huo wakimkashifu kwa maneno makali kuwa hangefaa kunyoa.

“Sina maoni hata, aliyewahi kukushauri kunyoa nywele angeweza kukupa kinyozi mzuri 🤣ukiwa mkubwa unashauriwa kunyoa lakini mtindo ni mbaya. Kumbuka una sura ya duara hivyo mtindo wa bob ungeweza kukutoa vizuri. Mimi ni kinyozi ndio maana nimeamua kuchangia maoni yangu,” mwingine alimzomea.

Baadhi walimtania kwamba ndio ameanza mapema kutoa muonekano mpya akijiweka tayari kwa maandalizi ya siku ya wapendanao wiki kesho.

Omanga ambaye ni mtetezi mkali wa rais William Ruto wiki jana alionekana akiwa nab inti yake Pwani wakijivinjari kwa shughuli mbalimbali za kustarehe.