Msanii mwenyekiti wa injili Guardian Angel ametuma ujumbe wa kimahaba kwa mke wake Esther Musila huku ulimwengu ukijumuika mitandaoni na kwenye sehemu za kujivinjari kuwaonesha wapendwa wao upendo wa kweli siku ya Valentino.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Guardian alipakia video akimsifia mkewe na kusema kwamab sit u mwezi Februari tarehe 14 anakumbuka mapenzi yake kwake bali ni kila siku tangu waoane mwaka mmoja uliopita.
Angel alisema kwamba ni muhimu kwa mtu kuonesha mapenzi yake mtu unayempenda.
“Kwangu mimi imekuwa siku na miezi ya kuoneshana mapenzi, si tu mwezi Februari ndio ninapata mapenzi. Mimi ninampenda mke wangu kila siku nikiamka kila asubuhi na kuangalia kando yangu na kuona urembo ambao Mungu ameniletea, ni jambo la kufariji moyo sana."
"Kila siku ni siku nzuri ya kuonesha upendo kwa watu wa karibu na wewe, kwa sababu watu wanasherehekea wanaowapenda mwezi huu, lakini ni vizuri kuwasherehekea uwapendao hata Zaidi ya huu mwezi..” Guardian Angel alisema.
Alimaliza kwa kumwambia Musila kwamba anampenda Zaidi ya jana n ahata siku moja hatokuja kujaa na kujutia maamuzi yake licha ya wenye midomo kulonga sana mitandaoni.
Musila kwenye picha ya Angel Instagram aliachia ujumbe wa kumhakikishia Angel upendo na kumwambia kwamba tangu akutane naye amembadilishia maisha yake kwa njia kubwa.
“Mpenzi wangu, umefanya maisha yangu kuwa ya ulimbwende mwingi,” Esther Musila alimjibu.
Wanandoa hao wamekuwa wakipigwa vita mitandaoni haswa kufuatia utofauti mkubwa uliopo baina ya umri wao, Musila akiwa na miaka 53 huku Guradian Angel akiwa miaka 20 nyuma yake kwa maana ya miaka 33.