logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rihanna hamfikii Zuchu hata kidogo - Mfanyikazi wa Diamond Platnumz asema

"Ule ukumbi angepewa @officialzuchu kiukweli wangesimuliana ..." - Diva.

image
na Radio Jambo

Makala14 February 2023 - 09:43

Muhtasari


• Kulingana na Diva, shoo ya Zuchu huko Sound City ilikuwa kubwa na ya kufurahisha zaidi kuliko ile ya Rihanna Super Bowl.

Rihana na Zuchu

Wikendi iliyopita msanii Rihanna alitumbuiza Super Bowl, tumbuizo ambalo limeendelea kuzungumzi kwenye mitandao ya kijamii.

Watu mbalimbali wametoa maoni yao huku baadhi wakimlinganisha na wasanii wengine na baadhi wakizungumzia kitumbo chake kuwa huenda ana mimba ya pili miezi kadhaa baada ya kupata mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake Asap Rocky.

Wakati Rihanna anatumbuiza Super Bowl, msanii Zuchu kutoka Tanzania pia alikuwa anatumbuiza kwenye tuzo za Sound City nchini Nigeria.

Sasa mtangazaji wa kituo cha redio cha Diamond Platnumz, Wasafi FM Diva Thee Bawse ameibua madai mapya kwamba Rihanna wakiwekwa na Zuchu kwenye ukumbi mmoja basi Rihanna atasahaulika kabisa.

Kulingana na Diva, Zuchu angepewa ile nafasi ya kupanda jukwaani huko Super Bawl, watu wangesimulia weledi wake, akisema kwamba licha ya kumkubali Rihanna lakini Zuchu alifanya vizuri kwenye Sound City kumliko.

“Rihanna Nnavyompenda .. ila Perfomance Ya Zuchu Sound City ilikuwa Kali kuliko Yake .. kwa kuanza na sijalala usiku kucha nikitazama ESPN halafu Jason Derulo kumaliza kidogo shoo kaenda mapumziko halafu Rihanna akaingia ukumbini... Ule ukumbi angepewa @officialzuchu kiukweli wangesimuliana ... Rihanna hakufanya kweli kama nilivyokuwa natarajia lakini alijaribu na inaeleweka sababu Ana Mimba ...” Diva alisema.

Kumkandia Rihanna akimpaisha Zuchu juu yake kulivutia hisia mseto kutoka kwa baadhi ya watu ambao baadhi walikubaliana naye na wengine walimcharukia kuwa anajileta kwangu kwangu kwa msanii wa WCB Wasafi kwa sababu anapigania ugali, asinge akazungumzia msanii wa bosi wake vibaya.

Diva kwa ghadhabu ya kuhisi kutukanwa naye alijibu mipigo kwa kusema kuwa wengi waliomkaripia kwa maneno makali ni wale ambao hawakuelewa kile alichokiandika kwa sababu alitumia lugha ya Kiingereza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved