logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee: Niombeeni nipate mimba upesi, umri hauko upande wangu

Mwishoni mwa mwaka jana, Akothee alitangaza kuharibikiwa na ujauzito.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri15 February 2023 - 06:59

Muhtasari


• Akothee alionesha nia yakec kupata mtoto mwingine wa 6 kabla kufikisha umri wa miaka 45.

Akothee aomba kupata mimba.

Msanii wa kizazi kipya anayetajwa kwenye mwenye mafanikio makubwa nchini, Akothee ammetoa wito kwa mashabiki wake mitandaoni kumweka kwenye maombi.

Msanii huyo ambaye mwishoni mwa mwaka jana alitangaza kupoteza ujauzito alisema anahitaji kupata mtoto kabla umri haujamuacha, na kuomba mashabiki kumuomba katika hilo.

Akothee mwenye umri wa miaka 42 anasema kwamba ana wasiwasi kuhusu umri wake kwenda kasi na huenda asifanikiwe kupata ujauzito baada ya kufikisha miaka 45 ambayo kisayansi mwanamke hana uwezo tena wa kushinda ujauzito.

Ombi lake kuu ni mpenzi wake mzungu aliyempa jina la Kiafrika kama Omondi kuitwa baba wakati mmoja na hilo litafanikishwa kupitia tumbo lake.

“Niombee nipate mimba upesi ,umri hauko upande wangu Omondi lazima awe baba ,kabla uchawi haujabadilisha mawazo 🤣🤣🤣 mitaa hii mmmm..” Akothee alitoa ombi kwa mashabiki wake.

Mjasiriamali huyo mama wa watoto watano mwishoni mwa mwaka jana kwa mfadhaiko mkubwa alitangaza kuharibikiwa ujauzito wake na mpenzi wake Omosh, jambo ambalo lilimfanya kuchukua mapumziko kutoka mitandaoni kwa muda.

Hivi majuzi, Akothee ameteuliwa na wizara ya vijana na spoti nchini kuwa miongoni wa wanabodi ya kusimamia vipaji na ubunifu nchini, bodi ambayo itaongozwa na mchekeshaji wa muda mrefu Daniel Ndambuki maarufu Churchill.

Akothee katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwaka jana, alisisitiza lengo lake la kupata mtoto wa mwisho kabla ya kufika miaka 45.

 Atakapofika miaka 45, Akothee aliorodhesha mipango yake ya kustaafu ambayo ni pamoja na kuhamia katika boma lake la kijijini na kuweka maisha yake faraghani mbali na mitandao ya kijamii.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved