Sitaki kuwa singo, si atokee mtoto wa mtu anipende jamani! - Esma Platnumz

Dadake Diamond alionea gere ndoa ya rafiki yake na kusema alimuaminisha kuwa ndoa kumbe ni kweli.

Muhtasari

• Esma amewahi kuwa katika ndoa mbili tofauti kwa nyakati vtofauti lakini zote zikabuma.

Esma atangaza anatafuta mwanamume wa kumuoa.
Esma atangaza anatafuta mwanamume wa kumuoa.
Image: Instagram

Dadake Diamond, Esma Platnumz ameweka wazi kuwa amechoka na maisha ya kuwa bila mpenzi na kusema kuwa anaomba mwanamume wa kumpenda atokee tu hivi karibuni.

Kupitia Instagram yake, Esma alikuwa anasifia rafiki yake mmoja aliyependwa na mwanamume mpaka kumbadilisha dini.

Alisema kuwa ndoa hiyo ya rafiki yake ilimpa taswira toafuti kabisa ya kuamini tena katika mapenzi licha ya kutendwa katika ndoa mbili na wanaume tofauti.

Esma ambaye ni Muislamu aliona jinsi rafiki yake alifanikiwa kumbadilisha mwanamume Mkristo hadi kukumbatia dini ya Kiislamu na kusema kuwa pia anataka Mkristo ili ambadilishe dini na wagandiane kwa mapenzi yasiyojua kufa.

“Si atokee mtoto wa mtu Mkristo anipende mpaka abadilishe dini kwa ajili yangu mjane mimi. Kumbe inawezekana, bwana sitaki usingo sasa, ajitokeze asilimu tu kwa kweli kwa ajili yangu,” Esma Platnumz alisema.

Esma amekuwa na bahati mbaya kkatika kidimbwi cha mapenzi huku akidai kuwa aliwahi wapenda wanaume wawili kwa nyakati tofauti hadi kuingia katika ndoa nao lakini matokeo yake mwisho wa siku ni kutendwa na kuishia kuumia na kuwa mnyonge.

Miezi michache iliyopita, Esma alipakia matokeo yake ya vipimo vya VVU vikionesha alikuwa hasi na kupiga bismillah akimshukuru Mungu kwa kumnusuru.