Mwigizaji Lenana na mkewe wafichua jinsia ya mtoto wao

Lenana na mkewe walifichua kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza mapema wiki hii.

Muhtasari
  • Mapema wiki hii Lenana alifichua kwamba mkewe anamshinda katika umri huku akifichua ana miaka 34 na mkewe 36

Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Selina Lenana Kariba kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua jinsia ya mtoto wake.

Kulingana na mwigizaji huyo wanatarajia mtoto msichana.

Lenana na mkewe walifichua kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza mapema wiki hii.

Lenana alisema;

Wikendi iliyopita familia yangu iliandaa baby shower ya ajabu kwa ajili yetu kusherehekea hatimaye kuwa na msichana mwingine kujiunga na genge (we are such a boy family 😂)... tulikuwa na wakati mzuri wa kusherehekea na wale wa karibu zaidi 🩷,"Aliandika Lenana.

Mapema wiki hii Lenana alifichua kwamba mkewe anamshinda katika umri huku akifichua ana miaka 34 na mkewe 36.

Mashabiki waliwapongeza wawili hao na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

anitanderu: Hongereni Honey Buns!!! nawafurahia wote  wasicha ni watoto wa ajabu❤️❤️❤️❤️

shikshaarora: Malkia mrembo zaidi anakuja, hongereni!!!!

mpweety_cortez: Timu wasichana, atakuwa mrembo zaidi 😍

gloshygyal: So both Patricia Mackenzie's sons wameamua to premier with girls. Nice! As a mother of 3 sons only this post has tickled my ovaries😊