logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rayvanny: Nina collabo nyingi na KRG ambazo hazijatoka, sijui tuanze na gani?

Mwaka jana, KRG alimualika Rayvanny katika klabu ya Casavera.

image
na Radio Jambo

Makala01 March 2023 - 08:12

Muhtasari


• "Nakuja tunaonana na tuna miradi mingi sana sasa hatujui tuanze na gani, kwa hiyo watu wasubiri,”  - Rayvanny.

Rayvanny kuachi collabo na KRG.

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Next Level kutoka Tanzania, Rayvanny amefichua kwamba ana miradi mingi ya muziki ambayo anapanga kufanya na msanii KRG the Don kutoka nchini Kenya.

Rayvanny alikuwa anazungumza na waandishi wa habari wa Kenya baada ya kutua katika uwanja wa JKIA usiku wa Jumanne.

Msanii huyoalilakiwa na KRG na alipoulizwa uhusiano wake na msanii huyo wa Kenya mwenye mikogo ya tausi, alisema ni undug utu ila akafichua japo kwa kiduchu kwamba wana kazi nyingi za pamoja ambazo wamekuwa wakishughulikia kwa muda na wameshindwa waanze kuachia gani.

“Mimi Kenya ni nyumbani, KRG ni ndugu yangu, ni familia yangu. Nakuja tunaonana na tuna miradi mingi sana sasa hatujui tuanze na gani, kwa hiyo watu wasubiri,” Rayvanny alisema.

Kwa upande wake KRG, alikejeli wale wanaosema hawajui muziki wake hata mmoja na kusema kwamba ni waliotumwa na mahasidi wake.

Msanii huyo pia alikanusha kwamba ngoma yake na Rayvanny ndio itakwua kubwa Zaidi, akisema kwamba amefanya mambo makubwa sana kwenye Sanaa ya muziki wa Kenya licha ya wengi kudai kwamba hawajui ngoma yake hata moja.

“Wale wamelipwa na maadui, yule jamaa ambaye anauliza watu ni mcheshi na alikuwa anaenda kwenye mtaa wenye hauna watu halafu anapanga watu wake kuwa wewe nendeni huko nikija nikuulize useme hujui,” KRG alisema.

Mwaka jana, KRG alimualika Rayvanny kwenye klabu ambayo anasema ni miliki yake Casavera iliyopo katika barabara ya Ngong jijini Nairobi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved