Msanii DNA afutilia mbali uwezekano wa kuoa maishani mwake, "sioni ikitokea!"

"Maisha yanakuja jinsi yanakuja na sijioni nimeishi na mwanamke eti tunashikana mikono tukitembea, hilo haliwezi kutokea kwangu,” DNA alisema.

Muhtasari

• Msanii huyo alisema aliwahi kuwa katika mahusiano mbali mbali lakini alihisi ni kama yeye ni mchafu zaidi kuwa katika uhusiano safi.

• Licha ya kutokana kuoa, DNA alisema kuwa bado watoto wake mabinti wanakuja kwanza hata kama hawezi kuwafanyia vitu ambavyo angependa kufanya kama baba.

DNA atoa kauli yake kuhusu kuoa.
DNA atoa kauli yake kuhusu kuoa.
Image: Facebook

Msani mkongwe wa Hip Hop nchini Kenya, DNA amefunguka kwamba katika maisha yake ya mbeleni haoni akikaa katika ndoa, katika kile alisema kuwa anahisi yeye ni mchafu sana kutulia katika muunganiko mwa mwnamke na mwanamume.

Msanii huyo alilazimika kuzungumzia hilo baada ya kukabiliwa na swali kwamba muda mwingi huwa anasikika akizungumzia sana masuala ya kibiashara lakini hajawahi sikika akizungumzia maisha yake katika kitivo cha mapenzi.

“Mimi nilianza na Hip Hop na lengo langu kuu lilikuwa kwa muziki tu wala sikuwa nafikiria kuhusu wanawake na mapenzi. Wanawake nilikuwa nawapotezea. Lakini katika maisha yangu nimekutana na wanawake wazuri na warembo, nimekuwa katika uhusiano wa muda mrefu… lakini kwa bahati mbaya huwa sipati sinia yote ya mapenzi,” msanii huyo alianza kufunguka sababu zake za kupotezea mapenzi.

DNA alisema kwamba anahisi kutofanikiwa kwake katika mapenzi nip engine anahisi ameharibika sana au hafai kuwa katika uhusiano wa mapenzi katika kile alikitaja kuwa mapenzi ni ya watu wa vijijini ambao hawajapata kuona picha kubwa ya maisha huku nje.

“Hizi stori za mapenzi ni za watu limbukeni. Watu wenye hawajaenda wakivunjwa mioyo huku na kule, nahisi kwamba mimi nilikuwa najua mengi Zaidi, nilikuwa na uzoefu mwingi ambao haungeniruhusu kuwa katika uhusiano safi. Mimi nilikuwa mchafu…” alisema kwa kujuta.

Msanii huyo alijutia kwamba hilo limemfanya kutokuwa na uwezo wa kuwapa watoto wake kile ambacho angependa kuwapa.

“Sasa, ukurasa mbaya katika hili ni kwamba sina uwezo wa kuwapa watoto wangu kile ningependa kuwapa, kama kukaa nao na kuwaona kila siku. Lakini maisha yanakuja jinsi yanakuja na sijioni nimeishi na mwanamke eti tunashikana mikono tukitembea, hilo haliwezi kutokea kwangu,” DNA alisema.

“Kadri ninavyojiangalia mwenyewe sasa, nahisi nguvu zangu ziko juu Zaidi ya kuwa na mtu mmoja tu. Ni kama nitampa wakati mgumu sana,” aliongeza.

Hata hivyo, msanii huyo alisema mapenzi yake kwa mabinti wake wawili bado hayawezi kubadilika na siku zote watakuja kwanza, hata kama hatoweza kukaa nao kila siku.