Ujumbe wa Francis Gachuri baada ya kupata kazi katika Serikali

Nimepaita mahali hapa nyumbani, nilipokuja hapa, nilikuwa kijana, ambaye sikuwa na familia wakati huo.

Muhtasari
  • Hii ni baada ya kuteuliwa kuwa Katibu, Mawasiliano ya Kimkakati chini ya kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa
MWANAHABARI FRANCIS GACHURI
Image: KWA HISANI

Mhariri mkuu wa siasa wa Citizen TV amewaaga mashabiki wake baada ya miaka 16 ya kuwa kwenye vyombo vya habari.

Hii ni baada ya kuteuliwa kuwa Katibu, Mawasiliano ya Kimkakati chini ya kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa

Mwanahabari huyo anasema anashukuru kwa nafasi nyingi alizopewa na vyombo vya habari.

"Mnamo tarehe 1 Septemba 2007, nilijiunga na RMS kama ripota wa siasa. Siku 5,660 baadaye, ninatangaza kuondoka ili kuchukua kazi nyingine ya kitaifa.

Ninashukuru na kunyenyekewa na uzoefu, masomo, na fursa nyingi ambazo nimepata katika tasnia

Nimepaita mahali hapa nyumbani, nilipokuja hapa, nilikuwa kijana, ambaye sikuwa na familia wakati huo.

Hatua zangu zote kuu zimetokea nikiwa hapa.Sasa nina familia mbili, mke wangu na watoto na vile vile familia ya RMS ambayo inajumuisha wenzangu, watazamaji wetu, wasikilizaji na wasomaji,"Alisema Francis.

Francis aliongeza zaidi;

"Namshukuru Mungu kwa kila jambo. Nina bahati adimu ya kufanya kazi na walio bora sana kwenye tasnia. Wenzangu ni bora zaidi. Ubora wa timu. Mwongozo wa thamani wa wakuu wangu utathaminiwa kila wakati," alisema.