Paula Kajala adokeza kuolewa, amtangaza mume mpya akitumia wimbo wa Rayvanny

"Mwamba huyu hapa," Paula alimtambulisha mume wake akimvisha pete.

Muhtasari

• Hivi majuzi, Rayvanny alidokeza kurudiana na Paula baada ya kauchana kwa mwaka mmoja.

Paula adokeza kufunga harusi.
Paula adokeza kufunga harusi.
Image: Instagram

Paula Kajala, binti wa mwigizaji mkongwe Kajala Masanja na ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki Rayvanny ametangaza kufunga harusi takatifu na mwanamume aliyemtambulisha kama Ally.

Kajala alipakia mfululizo wa picha hizo akiwa amevalia baibui ya samawati akivishwa pete na kutangaza rasmi kwamba ameondoka kwenye soko.

Alimshukuru mwanamume huyo Ally kwa kumpa heshima ya ndoa na kubadilika jina rasmi kuanza kujiita mke wa Ally.

“Ahsante mume wangu, mwamba huyu hapa,” Paula aliandika akitumia kiitikio cha wimbo mpya wa aliyekuwa mpenzi wake Rayvanny.

Hivi majuzi, Rayvanny alidokeza kurudiana na Paula kimapenzi baada ya wawili hao kuachana kimya kimya mwaka jana pasi n ahata mmoja wao kuzungumzia kilichojiri mpaka kuachana.

Paula aliweka wazi kwamba ameolewa na kuwataka watu kuendelea kufika kwenye duka lake ili kunuua nguo wakiendelea kusherehekea naye katika siku yake kubwa.

Hata hivyo, tumebaini kwamba Paula hakuwa amedokeza kwa njia yoyote kuhusu harusi hiyo yake, kinyume na ambavyo amekuwa akidokeza taarifa mapema kuhusu jambo lake kubwa lijalo.

Wengi walihisi kwamba hii ni kiki nyingine ambayo ametumia ili kusukuma mabo yake ya kibiashara ambapo alitangaza kuwa alikuwa na ofa ya kuuza katika duka la nguo la Paula Closet.

“Hii ni filamu nyingine. Hakuna kitu hapo, ni upepo mnatafuta,” mmoja alisema.

“Huu utakuwa uongo wa karne, halafu unatumia Wimbo wa ex wako eti mwamba huyu hapa,” mwingine alimwambia.