Produsa Martin Njoroge Kiptoo afanyiwa 'birthday' licha ya kuzaliwa Februari 29 (Video)

Kiptoo ni mzalishaji wa vipindi vya Gidi na Ghost asubuhi, Bustani la Massawe na vipindi vya michezo wikendi katika Radio Jambo.

Muhtasari

• Kiptoo alizaliwa Februari 29, tarehe ambayo huonekana mara moja kwa kila baada ya miaka minne tu.

• Katika mwaka wa 2023, tarehe hiyo haikuwa kwani Februari ilikamilika kwa siku 28.

Mzalishaji wa kipindi cha asubuhi katika kituo cha Radio Jambo, Martin Njoroge Kiptoo asubuhi ya Ijumaa alifanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na watangazaji wa kampuni ya Radio Afrika.

Shereeh hiyo ilikuwa ya aina yake nay a kipekee kwani produsa huyo alizaliwa Februari tarehe 29, tarehe amabyio haikuwa katika mwaka huu.

Katika kalenda ya kawaida, Februari 29 huja mara moja tu baada ya kila miaka mine, mwaka ambao unatajwa kuwa mrefu kwa kimombo ‘Leap year’.

Kiptoo alikuwa ametulia kwenye kiti chake baada ya kumaliza kuzalisha kipindi cha asubuhi cha Gidi na Ghost, katika kichwa chake akiwa amepotezea kabisa matumaini ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwani mwezi wa Februari ulishakamilika siku tatu zilizopita kwa siku 28 tu wala siku ya 29 ambayo ndiyo alizaliwa ikiwa haipo mwaka huu.

Watangazaji na wafanyikazi wa Radio Afrika wakiongozwa na mcheshi Oga Obinna walimkaribia na kumpiga bonge la ‘surprise’ ambapo kwa ghafla mno walianza kuimba viitikio vya nyimbo za kusherehekea siku ya kuzaliwa, Kiptoo alibaki na butwaa la kudumu kwenye paji la uso wake, asijue la kufanya.

Watangazaji hao walimtaka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya Februri 29 hata kama haiku, huku wakimkabidhi keki kubwa ambayo kwa mbwembwe alisimama na kuikata kabla ya kuwalisha wote waliokuwemo.