logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Unatoa nyimbo kila uchao lakini hunifikii," Diamond amlipua Harmonize bila huruma

Diamond alitazamwa mwezi Februari na wafuasi milioni 47 huku Harmonize akiwa na milioni 16.

image
na Radio Jambo

Habari03 March 2023 - 12:28

Muhtasari


• Sasa nyimbo zote unazozitoa kila kukicha faida yake ni gani? - Diamond aliuliza.

• Kwa mwezi Februari, Harmonize aliachia ngoma nyingi zikiwemo collabo.

Harmonize afurahia familia ya Diamond kucheza muziki wake

Bosi wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz amemlipua vikali  bila huruma adui wake mpya katika Sanaa ya Bongo Fleva, Harmonize.

Diaomond alipakia picha za chati za muziki wa Tanzania kwenye instastories zake na katika chati hizo, Harmonize ameongoza kwa wasanii waliotazamwa Zaidi mwaka huu licha ya kutoa ngoma tatu peke yake.

Katika chati nyingine, msanii huo alionesha jinsi lebo yake imekuwa ikitawala anga za muziki ambapo nyimbo tano kati ya nyimbo 10 kwenye orodha hiyo ni zile zimezalishwa katika lebo ya Wasafi na wasanii wake.

Alitumia fursa hiyo kutupa chokoza yake kwa Harmonize ambapo alimponda kwamba hana lolote na hawezi lazimisha ushindani naye wakati takwimu zinaonesha kuwa hawezi kumfikia hata atuame vipi.

Aliwataka wapinzani wake, haswa asilimia kubwa ikilenga kwa Harmonize kujikaza Zaidi ili angalau kuboresha ushindani kwani alikuwa mpweke kileleni mwa takwimu zote ambazo zilikuwa zinammlika yeye licha ya wasanii wengine kutoa ngoma kila uchao.

“Basi mnaolazimisha upinzani mngejikaza hata kidogo kwenye vimauzo vyenu jamani. Sasa nyimbo zote mnazotoa kila kukicha faida yake ni nini?” Diamond aliuliza.

Kwenye chati hiyo ya wasanii wa Tanzania waliotazamwa Zaidi mwezi Februari, Diamond anaongoza kwa watazamaji milioni 47 YouTube, akifuatiwa na Rayvanny na watazamaji milioni 20 huku Harmonize akifunga tatu bora na watazamaji Milioni 16.

Katika orodha hiyo ambayo ilikuwa imetawalwa na wasanii wa miziki ya kidunia, msanii Rose Muhando ndiye pekee alijinafasi katika nafasi ya saba katika wasanii 10 bora waliotazamwa Zaidi mtandaoni YouTube mwezi Februari.

Harmonize katika siku za hivi karibuni amekuwa akilazimisha ugomvi na Diamond, la hivi majuzi likiwa ni kutupa tuhuma na lawama kwa msanii huyo kuwa bado anaendelea kuchuma matunda ya wimbo wa Kwangwaru ambao alitoa kama collabo na Diamond kipindi ako chini ya lebo ya Wasafi.

Harmonize alisema licha ya kuhangaika juu chini na kutoa milioni 600 za Tanzania ili kupata uhuru wa hatimiliki za kazi ambazo alizifanya chini ya uongozi wa Wasafi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved