Andrew Kibe bila kunitukana hana kazi, na vile yeye ni maskini - Diana Marua

Andrew Kibe amekuwa akieneza uvumi kwamba Marua anamtawala mume wake Bahati.

Muhtasari

• “Andrew Kibe hakim bona unapenda kunitukana na vile wewe ni maskini?”

Marua amjibu Kibe
Marua amjibu Kibe
Image: Instagram

Diana Marua kwa mara ya kwanza amemjibu mwanablogu Andrew Kibe vikali kufuatia madai ambayo mwanablogu huyo mkaazi wa Marekani amekuwa akitupa kwa familia ya Maruac na mpenzi wake Bahati kwa muda mrefu sasa.

Kibe amekuwa akieneza uvumi kwamba Marua anamtawala Bahati na anamchukulia kama mtoto wake, kitu ambacho amekuwa akimtuhumu Bahati kwa kukubali kutawaliwa na mwanamke.

Kwa muda wote huu, familia ya Bahati na Marua haijawahi kumjibu Kibe lakii safari hii ni kama Kibe alikanyaga pabaya, mpaka kumghasi Marua ambaye amevunja kimya chake.

Kulingana na Marua, amegundua kwamba Kibe hawezi pata kitu cha kuzungumzia kwenye blogu yake ya YouTube pasi na kujadili kile ambacho kinaendelea katika familia yake.

“Nimegundua kuwa Bila kumtaja Diana B! huyu jamaa atakuwa hana Kazi 😂😂😂 ni sawa!” Diana Marua alizua.

Alizidi kwa kumsimanga vikali Kibe akisema kwamba yeye ni maskini sana kumliko, lakini haoni hilo bali kazi yake kumzungumzia kwa mabaya na chuki.

“Andrew Kibe hakim bona unapenda kunitukana na vile wewe ni maskini?” Diana Marua aliuliza kwa upole lakini kwa sauti iliyojawa kejeli na kebehi.

Kibe amekuwa akimzungumzia Marua kwa njia hasi, kumuita mzee kwa mume wake Bahati.

Lakini si yeye peke yake ambaye Kibe amekuwa akipiga mabomu ya moto. Mwanablogu huyo mwenye utata mwingi amekuwa akiwaingilia watu mashuhuri Kenya kwa njia ya aina yake, huku akionekana kufurahia kila mara watu hao wanapopatikana kwenye kashfa au skendo.

Baadhi ya wanamitandao walisema wangependa kumuona Kibe akijibu hilo, huku wakisema mwanablogu huyo atajibu kwa ukali kwani tayari ameshapata kitu cha kuzungumzia kwenye blogu yake.