DJ wa Tanzania acheza mziki juu ya mlima Kilimanjaro

Joozey ni mmoja wa wanamuziki wanaochipuka Tanzania.

Muhtasari

• DJ Joozey alicheza muziki wa dakika kumi na tano katika kilele cha mlima huo wenye urefu wa mita 5895

Image: BBC

Dj mmoja wa Tanzania amewashangaza watumiaji wa mtandao baada ya kusambaza video ambayo alikuwa akicheza muziki kwenye kilele cha mlima mrefu zaidi Afrika, Mlima Kilimanjaro.

Joseph Simo anayejulikana kwa jina maarufu kama DJ Joozey alicheza muziki wa dakika kumi na tano katika kilele cha mlima huo wenye urefu wa mita 5895

" Mimi ni mwanamume wa kwanza kuwahi kucheza seti ya DJ ya dakika 15. MUNGU NI MWEMA!” DJ alinukuu kipande cha video yake juu ya Mlima Kliimanjaro .

Joozey ni mmoja wa wanamuziki wanaochipuka Tanzania.

Kulingana na jarida la Tangaza Magazine, kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye tasnia ya showbiz kwa takriban miaka mitano.

Mwaka jana, DJ huyo alikuwa mmoja wa Waafrika wachache waliochaguliwa kushiriki katika kampeni ya albamu ya rapa wa Marekani DJ Khaled kwa ajili ya albamu yake ya ‘God Did’.