logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mfalme Charles anamwalika mtoto wake Harry, Meghan katika kutawazwa kwake

Harry na mkewe Meghan wamekuwacwakiishi Markani tangu kujitenga kutoka famialia hiyo.

image
na Radio Jambo

Makala06 March 2023 - 13:40

Muhtasari


• Mfalme Charles wa 3 anatarajiwa kutawazwa rasmi kama mfalme wa uingereza mwezi Mei.

• Kutawazwa kwake kunakuja baada ya kuchukua hatamu kutoka kwa Malkia Elizabeth wa pili aliyefariki mwaka jana.

Prince Harry na mkewe waalikwa katika kutawazwa kwa baba yake

Licha ya drama inayoendelea kati ya Prince Harry na Familia ya Kifalme ya Uingereza, Mfalme Charles III amemwalika mwana wa mfalme huyo aliyejihami na mkewe, Megan Markle, kuhudhuria hafla ya kutawazwa kwake mwezi Mei.

Msemaji wa wanandoa hao alithibitisha habari hizo kwa gazeti la The Times, Uingereza siku ya Jumamosi, akisema kwamba "Ninaweza kuthibitisha kwamba Duke amepokea barua pepe hivi karibuni kutoka kwa ofisi ya mflame Charles kuhusu kutawazwa."

Mwaliko huo unakuja huku kukiwa na mwito wa hadharani wa wanandoa hao dhidi ya Ufalme wa Uingereza katika siku za hivi karibuni.

Wanandoa hao walihamia Marekani mnamo 2020 baada ya kujiuzulu kama Wakuu wa familia ya Kifalme. Tangu wakati huo wamepokea watoto wawili, Archie na Lilibet.

Mnamo 2021, Harry na Megan walifanya mahojiano ya kushangaza na Oprah Winfrey, ambapo waliwashutumu washiriki wasio na majina wa familia ya kifalme kwa ubaguzi wa rangi.

Wanandoa hao walitoa filamu ya Netflix mnamo Desemba 2022, ikielezea uzoefu wao mbaya kama washiriki wa familia ya kifalme baada ya ndoa yao mnamo 2018.

Harry pia hivi karibuni alitoa tawasifu ya yake ambapo alimwaga ubuyu wote kuhusu uhusiano ulioharibika baina yake ya wanafamilia wengine katika familia ya kifalme inayoishi kwenye kasri la Buckingham.

Chapisho la Januari 2023 lilikuwa na madai ya Harry kwamba kakake mkubwa Mwana-mfalme William alimshambulia wakati wa mabishano kuhusu Meghan, na kwamba ugomvi huo ulizidisha uhusiano wao kuwa na nyufa Zaidi.

Katika kile kinachoonekana kama kulipiza kisasi na Ikulu ya Kifalme, Harry na Meghan walitakiwa kuondoka Frogmore Cottage, nyumba yao ya Uingereza, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wakati Mfalme amewaalika wanandoa hao waliojitenga kutoka shughuli zozote za Ufalme wa Uingereza, kwenye kutawazwa, haijulikani ikiwa wanandoa hao watahudhuria hafla hiyo. Mwakilishi wao aliiambia Times kwamba, "uamuzi wa mara moja juu ya kama Duke na Duchess watahudhuria hautafichuliwa nasi kwa wakati huu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved