"Wewe ni kila kitu nilichoomba na zaidi!" Mwimbaji Bien amsherehekea mkewe kimahaba

Bien alimweleza mkewe jinsi anavyojivunia na kufurahia sana kuwa naye maishani.

Muhtasari

โ€ขBien na Chiki walifunga pingu za maisha kwa siri mnamo mwezi Machi 2020 katika harusi ndogo ambayo haikutangazwa sana.

โ€ข"Safari yetu iliyosalia ijazwe na vicheko na machozi ya furaha. ๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน Nakupenda," alisema.

Bien na Chiki Kuruka
Image: INSTAGRAM// BIEN

Mwimbaji wa bendi ya Sauti Sol, Bien aime Baraza na mkewe Chiki Kuruka waliadhimisha miaka mitatu ya ndoa yao siku ya Jumatatu, Machi 6.

Bien na Chiki walifunga pingu za maisha kwa siri mnamo mwezi Machi 2020 katika harusi ndogo ambayo haikutangazwa sana.

Mwanamuziki huyo mahiri alitumia siku hiyo maalum kwao kumsherehekea kimahaba mkewe ambaye pia ni meneja wake rasmi na kumweleza jinsi anavyojivunia na kufurahia sana kuwa naye maishani.

"Kheri ya kumbukumbu ya ndoa Chiki Kuruka. Asante kwa kuwa mtu wangu. Ninashukuru sana kuwa na wewe katika maisha yangu," alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatatu.

Bien alibainisha kuwa Chiki ana sifa zote ambazo alitaka kwa mke.

Aidha, alimhakikishia mke wake kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na akaomba neema juu ya ndoa yao.

"Safari yetu iliyosalia ijazwe na vicheko na machozi ya furaha. ๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน Nakupenda," alisema.

Harusi ya kupendeza ya wanandoa hao ilifanyika Pallet Cafe katika mtaa wa Lavington. Chanzo cha karibu kilisema ilikuwa harusi ya bustani ambapo watu wapatao 150-200 pekee walialikwa kuhudhuria.

Waliohudhuria ni pamoja na wanabendi ya Sauti Sol; Willis Chimano, Savara Mudigi, na Polycarp Otieno pamoja na waimbaji wengine maarufu kama vile Nyashinski na Nameless miongoni mwa wengine.

Bien ana tattoo kwenye kidole chake cha pete ambayo anasema inatumika kama pete ya harusi.

Kwenye mahojiano na SpmBuzz, Bien alisema alipoteza pete yake halisi ya ndoa na kuchagua kuchorwa tattoo ya pete kama mbadala wa kudumu. Alisema ana uhusiano mbaya sana na vitu na pengine ndiyo sababu na jinsi alivyoishia kupoteza pete yake ya ndoa.

"Nilipoteza pete yangu halisi! Nilikuwa nayo lakini ilipotea na nikachagua kuwa na tattoo badala yake kwa sababu haitaenda popote na pia ninahisi nina uhusiano mbaya na vitu," alisema

Aliongeza, "Nahisi huwezi kuambatanisha thamani ya kitu. Watu hukasirika wanapoona wapenzi wao hawana pete zao za ndoa, kwa nini? Sio mbwa unawatia kamba."