Mnamo 2021 a familia ya Wajesus iligonga vichwa vya habari kwenye mitandao yote ya kijamii kuhusiana na madai kuwa Kabi hamsaidii mtoto wake.
Aliyepasua mbarika ambaye ni binamu ya Kabi alisema kwamba alipuuza majukumu yake kama baba kwa mtoto wao.
Drama hiyo kwa hakika ilileta msukosuko kwenye familia ya wanandoa hao wawili.
Wakizungumza kwenye chaneli yao ya YouTube kwa jina 'Wajesus Family' Peter Kabi almaarufu Kabi Wajesus na Millicent Wambui almaarufu Milly Wajesus walikuwa na mazungumzo ya wazi na mashabiki wao kuhusu ndoa yao.
Kabi Wajesus alifichua kuwa Milly alipoteza imani naye. Yeye huwa na wasiwasi juu ya kile anachofanya wakati hawako pamoja.
"Mimi hufeel nikama ulichange. Kuna scandals fulani zilikam kwa life nikaona nikama maybe unataka sasa kujua exactly kila kitu. Kuna ka honesty fulani kalikutoka; ka trust. Nafeel nikama tangu hio drama iktokee unataka kuskia vizuri kila kitu. Nakwambia nilikuwa mahali fulani you feel like I nahitaji kukuambia ukweli wote kila wakati. Ndivyo ninahisi"
Milly aliongeza kuwa imani inatolewa Wakati mtu anajionyesha kuwa hafai anahoji imani yake.
"Uaminifu hupatikana. Umewahi kusikia siri huko nyuma. Sina siri zinazoweza kukuathiri,au kuniathiri nina siri zangu binafsi."