Najisherehekea kwa kutambua changamoto nakabiliana nazo - Edday Nderitu, mke wa Smidoh

Eddya aliandika ujumbe weney nguvu kwa wanawake wote huku dunia ikisherehekea siku ya wanawake.

Muhtasari

• Wanawake wana jukumu muhimu zaidi katika kujenga na kusawazisha jamii yoyote. - Neritu.

Edday Nderitu, mke wa Samidoh.
Edday Nderitu, mke wa Samidoh.
Image: Facebook

Mke wa kwanza wa mwanamuziki Samidoh, Edday Nderitu amejitungia ujumbe wa kujiliwaza na wakati huo huo kujisherehekea huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wanawake.

Nderitu ambaye wiki mbili zilizopita aligonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba alikuwa amechoka kuteswa katika mapenzi na msanii Samidoh, na kwamba alikuwa anatathmini hatua ya kuvunja uhusiano wao alisema kwamba siku hii ya wanawake duniani anaisherehekea pamoja na wanawake wengine ambao wanazitambua changamoto wanazokabiliana nazo kila siku.

“Kheri ya Siku ya kimataifa kwa Wanawake, tulianza kutoka mahali fulani na shukrani kwa kila mtu hapa! Katika siku hii nachagua kusherehekea kila mwanamke na mimi kwa mafanikio na kutambua changamoto tunazoendelea kukabiliana nazo siku hadi siku,” Nderitu aliandika.

Alizidi kuelezea umuhimu wa mwanamke katika jamii na dunia kwa ujumla, akisema kwamba mwanamke ni kiungo maalum katika ulimwengu na bila wao, basi ladha ya maisha haingehisika kabisa.

“JAMII bila wanawake si kitu. Dunia bila wanawake si kitu. Wanawake wana jukumu muhimu zaidi katika kujenga na kusawazisha jamii yoyote. Kuanzia kufanya kazi majumbani hadi kufanya kazi maofisini, wanawake hutengeneza mustakabali wa jamii au nchi yoyote!” Nderitu alitema lulu.

Mpaka sasa, haijulikana iwapo mwanamama huyo aliondoka katika uhusiano wake na Samidoh wa miaka 15 au bado wanaishi pamoja.

Nderitu na Samidoh wana watoto watatu na alifichua kwamba walikuwa wameishi kama mke na mume kwa miaka 15 iliyopita.

Baadae baada ya Samidoh kupatana na seneta Karen Nyamu na kuzama kwenye poenzi zito, walizaa watoto wawili, jambo ambalo halijakuwa likimfurahisha mke wa kwanza tangu mwaka 2021 uhusiano wao ulipojulikana bayana.