logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nitajirekebisha niwe rafiki bora kwako" Boniface Mwangi amuahidi mkewe wakiadhimisha miaka 15 ya ndoa

Mwangi alitumia fursa hiyo kumhakikishia Bi Njeri kuhusu mahaba yake mazito kwake.

image
na Radio Jambo

Habari08 March 2023 - 04:37

Muhtasari


•Mwangi alibainisha kuwa ndoa yao imekuwa safari nzuri na akaweka wazi kuwa iwapo angerudi nyuma basi hangesita kumchagua tena Bi Njeri kama mwenza wake wa maisha.

•Njeri alimshukuru mumewe kwa kuwepo kila siku kwa ajili yake na kwa upendo wake mkubwa kwa familia yao.

Mwanaharakati mashuhuri Boniface Mwangi na mke wake Hellen Njeri Mwangi waliadhimisha miaka kumi na tano ya ndoa yao siku ya Jumanne, Machi 8.

Wanandoa hao ambao wamekuwa pamoja kwa miaka 17 walifunga pingu za maisha mnamo Machi 8, 2008 katika harusi ya kufana.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumanne, Mwangi alibainisha kuwa ndoa yao imekuwa safari nzuri na akaweka wazi kuwa iwapo angerudi nyuma basi hangesita kumchagua tena Bi Njeri kama mwenza wake wa maisha.

"Miaka 15 iliyopita siku kama hii (Machi 8), tulifunga ndoa. Imekuwa safari nzuri, na ikiwa ningerudi nyuma tena, na kuchagua ambaye nitakatumikia maisha yangu yote naye, bado ingekuwa wewe," aliandika kwenye Instagram.

Mwanaharakati huyo aliambatanisha ujumbe wake na picha ya kumbukumbu ya siku ambayo walifunga pingu za maisha.

Alitumia fursa hiyo kumhakikishia Bi Njeri kuhusu mahaba yake mazito kwake.

"Kheri ya siku ya ukumbusho wa ndoa mpenzi wangu @njerikan. Naahidi kujifanyia kazi kwa bidii, ili niwe rafiki mzuri zaidi," alimwambia mkewe.

Njeri alibainisha kuwa miaka 15 ya ndoa yao imekuwa ya kusisimua na kufichua kuwa wameweza kufanikisha mengi.

Pia alimshukuru mumewe kwa kuwepo kila siku kwa ajili yake na kwa upendo wake mkubwa kwa familia yao.

"Tulichukua hatua na kusema "Ndio". Tumefanya mengi sana. Imekuwa msisimko, tukio la kweli, kupitia na kupitia 🙏🏾. Asante kwa kutuamini, kwa kujaribu kila wakati, kwa kutokukata tamaa nasi, kwa kurudi kila mara tunapoyumba, kwa kunipenda hata inapoonekana kuwa rahisi kutonipenda. Asante kwa kunichagua, tena na tena…na tena. Baada ya YOTE tumepitia, bado nakuchagua🙌🏾," alisema.

Njeri alimtakia mumewe kheri ya siku ya ukumbusho wa ndoa  na kuutakia muungano wao maisha marefu zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved